Sunday, November 24

Fahamu miji ya kale yenye majumba marefu nchini Yemen

Mijengo ya kale

CHANZO CHA PICHA,MACIEJSTANGRECIAK/GETTY IMAGES

Ikiwa imejengwa kwa vifaa asilia, mijengo mirefu ya Yemen inafaa kikamilifu kwa hali ya hewa ya joto kwa jangwa la Arabia.

Kupitia Bab-al-Yaman, lango kubwa linaloruhusu kuingia katika jiji la kale linalozungukwa na kuta la Sana’a nchini Yemen, ilikuwa ni kama kupita lango kuingia katika ulimwengu mwingine. Majengo marefu, membamba yaliyosongamana kwenye barabara nyembamba zilizounganisha bustani za matunda na mboga mboga ambapo punda bado wanauzwa.

Niliona mafundi wa kufuli wakitengeneza funguo kubwa za chuma ambazo hufungua milango ya mbao yenye nguvu; mchuuzi anayeuza pears kutoka kwa mkokoteni, na mwokaji ,akivuta mkate kutoka kwenye shimo linalowaka moto ardhini. Katika chumba kidogo, ngamia alizunguka akisukuma jiwe la kusagia nafaka

Lakini licha ya kuona yote hayo, ni usanifu uliojitokeza zaidi.

Sanaa imejaa majengo tofauti kabisa na mahali pengine popote duniani. Kwenye barabara, ambapo kuta za matofali ya udongo hutenganishwa tu na milango mikubwa ya mbao, mara nyingi hakukuwa na mengi ya kuona.

Lakini nilipotazama juu, niligundua majengo haya membamba, mengine yenye chumba kimoja au viwili kwa kila ghorofa, yalipaa juu angani.

Wakati orofa za chini, karibu na barabara hazikuwa na madirisha kwa sababu ya matumizi yake kama malazi ya wanyama au sehemu za kufanyia kazi, madirisha yenye mapambo yaliyo juu zaidi yalifunikwa na vioo vya rangi au skrini maridadi za mashrabiya zinazolinda usiri wa wanawake ndani.

Mengi yalikuwa na paa, ambazo zilitumiwa pia kama nafasi za burudani na pia vyumba vya kulala vya nje usiku wa joto. Uzuri wa majengo, viliyafanya kuwa na muoenekano wa usanifu ulioridhisha.

Nilipanda juu ya paa la ghorofa ya saba ambalo lilikuwa limegeuzwa kuwa mgahawa; Mji Mkongwe ulikuwa chini yangu, lakini majengo jirani yalikuwa marefu kama lile nilikuwa nimesimama juu yake, na hivyo kuibua hisia kuwa nilikuwa nimezungukwa na majumba marefu.

Ningehisi kuwa nilikuwa mahala kama Dubai au New York, ijapokuwa ujenzi huu ulikuwa wa tangu miaka 300 na 500 iliyopita na ulifanywa kutoka kwa matope.

Baadhi ya majumba marefu ya Yemen yanaweza kufikia urefu wa takriban mita 30, na majumba marefu ya kwanza ya kisasa huko Chicago yalikuwa marefu kidogo tu kuliko hayo.

Inajulikana kama "Manhattan ya Jangwani", jiji la Shibam la karne ya 16 lilipewa hadhi ya Urithi wa Dunia mnamo 1982.

CHANZO CHA PICHA,DAVORLOVINCIC/GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Inajulikana kama “Manhattan ya Jangwani”, jiji la Shibam la karne ya 16 lilipewa hadhi ya Urithi wa Dunia mnamo 1982.

Mtindo wa usanifu wa majengo marefu wa Yemen ni wa kipekee sana hivi kwamba miji ya Zabid, Shibam na mji mkongwe wa Sana’a imetambuliwa kama maeneo ya kihistoria na shirika la Unesco, huku mila hiyo ikikadiriwa kuanzia Karne ya 8 na 9, kulingana na Trevor Marchand, profesa wa anthropolojia ya kijamii katika chuo cha Oriental and African Studies (SOAS) mjini London.

Kinachofanya majumba marefu ya Yemen kuwa ya kipekee zaidi ni kwamba bado yanatumika, kama yalivyokuwa mamia ya miaka iliyopita. Mji Mkongwe wa Sana’a, kwa mfano, ingawa majengo machache yamegeuzwa kuwa hoteli na migahawa, mengi bado zyanatumika kama makazi ya watu binafsi.

“Kama watoto, tungecheza mpira kwenye vichochoro na kama vijana tulikuwa tunakunywa kahawa chini ya kioo chenye rangi,” alisema Arwa Mokdad, mtetezi kwenye wakfu wa ujenzi mpya nchini Yemen.

Nilipokuwa nikizunguka nchi nzima, nikistaajabia miji hii yenye mijengo mirefu, sikujizuia kujiuliza kwa nini watu wa Yemen walijenga majumba haya marefu, ukizingatia eneo kubwa la jangwa la nchi yao.

Salma Samar Damluji, mbunifu na mwandishi wa usanifu wa Yemen na ujenzi upya alisema kwamba ujenzi, ulikuwa wa kawaida kwa maeneo madogo, kumaanisha majengo yanahitajika kuwa marefu. “Miji na majiji yalikuwa na ukuta za nje, zinazoitwa Sur, na mpaka wa nje kutoka kwa jangwa,” alisema,

Ilikuwa pia hitaji la ulinzi ambalo lilifanya makazi ya Yemen kuwa pamoja badala ya kutawanyika. Kuishi katika jangwa lisilo na usalama na uwezo wa kutazama nje ya nchi kwa maadui wanaokaribia, pamoja na uwezo wa kufunga milango ya miji usiku, ilibidi vizingatiwa katika mipango yoyote ya miji.

Kasri kubwa Dar al-Hajar nchini Yemen limejengwa juu ya mwamba wa asili.

CHANZO CHA PICHA,CRAIG PERSHOUSE/GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Kasri kubwa Dar al-Hajar nchini Yemen limejengwa juu ya mwamba wa asili.

“Sababu muhimu iliyochangia katika historia ya Yemen ya majengo marefu ilikuwa hitaji la usalama dhidi ya vikosi vinavyovamia, na vile vile wakati wa migogoro ya kikabila au vita vya wenyewe kwa wenyewe,” Marchand alielezea.

Ikiwa imejengwa kwa vifaa asilia, mijengo mirefu ya Yemeni inafaa kikamilifu kwa hali ya hewa ya joto na kavu ya jangwa la Arabia. Maeneo ya paa pia hutumiwa kama vyumba vya kulala vilivyo nje, huku skrini kwenye madirisha zikiruhusu hata upepo mdogo kuingia ndani ya nyumba, huku pia ikiruhusu mwanga lakini si joto jingi.

Wajenzi wangeanza na msingi wa mawe, mara nyingi kina cha mita 2, ambapo matofali ya udongo yaliwekwa kwenye mtaro, kumaanisha tofali moja lililaliwa na matofali mawili.

Kisha walijenga polepole kuelekea juu, wakiweka vifaa vya mbao kwa nguvu na kuongeza sakafu zilizotengenezwa kwa mbao na vifaa vya mawese walipokuwa wakipanda juu.

Hata hivyo, kulingana na Damluji, ujuzi huu wa unakaribia kutoweka. “Tunaangalia miundo ambayo inaweza kudumu hadi miaka 300 na zaidi. Majengo ya ghorofa sita au saba yaliyojengwa kwa matofali ya udongo yaliyokaushwa na jua kwa njia ambayo hakuna msanifu wa kisasa anayeweza kujenga hivyo.”

Inajulikana kama "Manhattan ya Jangwani", jiji la Shibam la karne ya 16 lilipewa hadhi ya Urithi wa Dunia mnamo 1982.

CHANZO CHA PICHA,DAVORLOVINCIC/GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Inajulikana kama “Manhattan ya Jangwani”, jiji la Shibam la karne ya 16 lilipewa hadhi ya Urithi wa Dunia mnamo 1982.

li kuzuia ujuzi huu usipotee, Damluji hufanya kazi kwa karibu na Taasisi ya Usanifu wa Dawan, ambayo inajitahidi kuhifadhi mbinu hizi za ujenzi, ikihimiza matumizi ya vifaa na mbinu za jadi kuliko mitindo ya kisasa.

Majengo haya ya kihistoria pia yanakabiliwa na tishio la mmomonyoko wa mara kwa mara, vita na ugumu wa kiuchumi ambavyo huzuia familia kutunza nyumba zao ipasavyo.

Mnamo mwaka wa 2020, Unesco ilikagua takriban majengo 8,000 na kurejesha 78 ambayo yalikaribia kuporomoka. Unesco inafanya kila iwezalo kuokoa majengo mengi iwezekanavyo, lakini ni ngumu katika mazingira ya sasa.

“Ni tukio la kuhuzunisha kushuhudia historia ikigeuka kuwa kifusi,” Mokdad alisema. “Uharibifu huu ni mkubwa”

“Mahali pengine, majengo haya yangekuwa makumbusho, lakini nchini Yemen yanabaki kuwa makazi. Siwezi kuanza kuelezea fahari ya kuishi katika nyumba iliyohifadhiwa na vizazi vya mababu zetu – ni uhusiano wetu na siku za nyuma.” Aliongeza.