Ilichukua miaka 375 kwa wanasayansi kugundua bara la nane duniani, ambalo limekuwa likijificha sehemu ya wazi muda wote. Lakini bado kuna fumbo halijawekwa wazi.
Ilikuwa mwaka 1642 na Abel Tasman alikuwa kwenye kazi maalumu. Baharia mzoefu wa Uholanzi mwenye sharubu zenye mbwembwe na ndevu nyingi lakini i pia alikuwa ni mpenda haki. Alikuwa na uhakika wa kuwepo kwa bara kubwa katika kusini mwa dunia na aliamua kulitafuta.
Wakati huo, sehemu hii ya dunia ilikuwa bado haijulikani kwa Wazungu, lakini walikuwa na imani thabiti kwamba lazima kutakuwa na ardhi kubwa huko ambayo iliitwa Terra Australis. Ili kusawazisha bara lao la Kaskazini, Marekebisho hayo yalianza nyakati za Warumi wa Kale, lakini sasa tu ndio yanakwenda kujaribiwa.
Na mnamo Agosti 14, Tasman alisafiri kutoka kituo cha kampuni yake huko Jakarta, Indonesia, akiwa na meli mbili ndogo na kuelekea magharibi, kisha kusini, mashariki na mwishowe akaishia kwenye Kisiwa cha Kusini cha New Zealand.
Kukutana kwake kwa mara ya kwanza na watu wa Wamaori (ambao wanadhaniwa waliishi hapo karne kadhaa zilizopita) hakukuenda vizuri, siku ya pili, mitumbwi kaadha ilipata hitilafu na kugonga mashua ndogo iliyokuwa ikisafirisha ujumbe kati ya meli za Uholanzi. Wazungu wanne walifariki. Baadaye, Wazungu walirusha mizinga kwa mitumbwi 11 zaidi – haijulikani ni nini kilifanyika kwa malengo yao.
Na huo ndio ukawa mwisho wa misheni yake Tasman alilipa jina la eneo la pwani ya wauaji, kwa utani tu na akasafiri kwa meli hadi nyumbani wiki kadhaa baadaye bila hata kukanyaga ardhi hii mpya. Ingawa aliamini kwamba kweli alikuwa amegundua bara kuu la kusini, ni dhahiri, haikuwa hali ya kibiashara ambayo alikuwa amefikiria. Hakurudi.
Mnamo mwaka wa 2017, kikundi cha wanajiolojia waligonga vichwa vya habari walipotangaza ugunduzi wao wa Zealandia -Te Riu-a-Māui katika lugha ya Kimaori. Bara kubwa la maili za mraba milioni 1.89 (kilomita za mraba milioni 4.9) ni karibu mara sita ya ukubwa wa Madagaska.
Ingawa ensaiklopidia za ramani na utafutaji zimekuwa zikisisitiza kwamba kuna mabara saba tu kwa muda, timu hiyo iliufahamisha ulimwengu kwa ujasiri kwamba hii haikuwa sawa. yapo nane hata hivyo na maelezo ya hivi karibuni yamevunja rekodi zote kwa kuongeza kuwa ni dogo zaidi, jembamba na changa zaidi ulimwenguni. Jambo inaelezwa kuwa 94% ya bara hilo iko chini ya maji na visiwa vichache tu, kama vile New Zealand, kutoka kwenye vilindi vya bahari Ilikuwa imejificha mahali pa wazi muda wote.
Huu ni mfano wa jinsi jambo dhahiri linaweza kuchukua muda kuonekana,” anasema Andy Tulloch, mwanajiolojia katika Taasisi ya Utafiti wa New Zealand GNS Science, ambaye alikuwa sehemu ya timu iliyogundua Zealandia.
Lakini huu ni mwanzo tu, Miaka minne na kuendelea na bara ni kama fumbo tangu zamani, siri zake zinalindwa chini ya futi 6,560 (2km) ndani ya maji. liliundwaje? Nini aliishi zamani huko? Na limekuwa chini ya maji kwa muda gani?
Ugunduzi mgumu
Kwa kweli, Zealandia imekuwa ngumu kusoma kila wakati.
Zaidi ya karne moja baada ya Tasman kuvumbua New Zealand mwaka wa 1642, mtengenezaji wa ramani Mwingereza James Cook alitumwa katika safari ya kisayansi kwenye ulimwengu wa kusini. Maagizo yake rasmi ilikuwa ni kuangalia kupita kwa sayari ya Venus, ili kukokotoa umbali wa Jua.
Lakini pia alibeba bahasha iliyofungwa, ambayo aliagizwa kuifungua akimaliza kazi ya kwanza. Hii ilikuwa na ujumbe wa siri wa juu wa kugundua bara la kusini ambapo bila shaka alisafiri kwa meli moja kwa moja, kabla ya kufika New Zealand.
Vidokezo halisi vya kwanza vya kuwepo kwa Zealandia vilikusanywa na mwanasayansi wa asili wa Scotland Sir James Hector, ambaye alishiriki katika safari ya kuchunguza mfululizo wa visiwa kwenye pwani ya kusini ya New Zealand mwaka wa 1895. Baada ya kujifunza jiolojia yao, alihitimisha kwamba New Zealand ni ” mfulizo wa milima ambao uliunda eneo kubwa la bara lililoenea hadi kusini na mashariki,na ambalo sasa limezam”.
Kisha katika miaka ya 1960, wanajiolojia hatimaye walikubaliana juu ya ufafanuzi wa nini maana ya bara kwa upana, eneo la kijiolojia na mwinuko wa juu, aina mbalimbali za miamba na ganda nene. Inapaswa pia kuwa kubwa. “Huwezi kuwa na kipande kidogo,” anasema Mortimer. Hii iliwapa wanajiolojia kitu cha kufanya kazi, ikiwa wangeweza kukusanya ushahidi, wangeweza kuthibitisha kwamba bara la nane lilikuwa halisi
Bado ilikwama kwani kugundua bara ni ngumu na ni ghali, na Mortimer anaonyesha kuwa hakukuwa na dharura. Mwaka 1995, mwanajiofizikia wa Amerika Bruce Luyendyk alielezea tena eneo hilo kama bara na akapendekeza kuiita Zealandia. Kuanzia hapo, Tulloch anaelezea ugunduzi wake kama ni kitu kinachoendelea kukua.
Wakati huo huo, “Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria ya Bahari” ulianza kutumika, na hatimaye ulitoa motisha kubwa. Inasema kuwa nchi zinaweza kupanua maeneo yao ya kisheria zaidi ya Eneo lao la Kiuchumi katika bahari, ambalo hufikia maili 200 za baharini (370km) kutoka ukanda wa pwani zao, ili kudai eneo la bara lililopanuliwa pamoja na utajiri wote wa madini na mafuta.
Ikiwa New Zealand inaweza kuthibitisha kuwa ilikuwa sehemu ya bara kubwa, inaweza kuongeza eneo lake kwa mara sita. kulikuwa na fedha nyingi kwa ajili ya safari za kuchunguza eneo hilo na ushahidi uliongezeka. katika kila sampuli ya miamba iliyokusanywa, vilienda kuboresha mazingira ya suala la Zealandia
Wakati bara hili lilipowekwa wazi hatimaye, lilifungua moja ya maeneo makubwa zaidi ya baharini duniani. Mortimer anasema, “Ikiwa unafikiria juu yake, kila bara kwenye sayari ina nchi tofauti juu yake, lakini kuna maeneo matatu pekee kwenye Zealandia.”
Upanuzi wa ajabu
Hapo awali, Zealandia ilikuwa sehemu ya bara kuu la kale la Gondwana, ambalo liliundwa miaka milioni 550 iliyopita na kimsingi liliunganisha ardhi yote katika ulimwengu wa kusini. Ilichukua kona upande wa mashariki, ambapo ilipakana na zingine kadhaa kama Magharibi ya Antaktika Magharibi na Australia yote ya mashariki.
Kisha karibu miaka milioni 105 iliyopita, “kutokana na mchakato ambayo hatuelewi kabisa, Zealandia ilianza kusukumwa mbali,” anasema Tulloch.
Zealandia iliishia kuvutwa kiasi kwamba sehemu ya safu ya juu imetanuka hadi kilometa 20 (maili 12.4) kwenda chini na hatimaye bara hilo jembamba lilizama ingawa halikufikia kiwango cha safu wa kawaida wa bahari na kutoweka chini ya bahari
Licha ya kuwa nyembamba na chini ya maji, wanajiolojia wanajua kwamba Zealandia ni bara kwa sababu ya aina za miamba inayopatikana huko.
Lakini bado kuna mengi yasiyojulikana Kwa mfano, bado haijulikani wazi jinsi Zealandia iliweza kukaa pamoja wakati ilikuwa nyembamba na haikugawanyika katika mabara madogo madogo.
Mjadala kuhusu dinosaria
Ni miongoni mwa mabaki ya wanyama adimu katika ulimwengu wa kusini lakini mabaki kadhaa yalipatikana New Zealand katika miaka ya 1990 ikiwa ni pamoja na mfupa mkubwa wa mbavu wa dinosauria mwenye mkia mrefu, shingo ndefu (sauropod) na dinosaur wa kivita (ankylosaur).
Kisha mwaka wa 2006, mfupa wa mguu wa wanyama wanaokula nyama mkubwa, pengine aina ya allosaur, uligunduliwa katika Visiwa vya Chatham, takriban maili 500 (800km) mashariki mwa Kisiwa cha Kusini. Muhimu zaidi, wanyama wote hao waligunduliwa baada ya bara la Zealandia kugawanyika kutoka kwa Gondwana
Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa kulikuwa na dinosauria waliokuwa wakizurura katika sehemu kubwa ya Zealandia – “Kuna mjadala mrefu kuhusu hili, kuhusu kama inawezekana kuwa na wanyama wa nchi kavu bila ardhi,” anasema Rupert Sutherland, Profesa wa Jiofizikia na Tectonics katika Chuo Kikuu cha Victoria cha Wellington.
ingawa haiwezekani kukusanya masalia kutoka bahari ya Zealandia moja kwa moja, wanasayansi wamekuwa wakitengeneza kina chake kwa kuchimba visima. “Kwa kweli mabaki ya kusaidia zaidi na ya kipekee ni yale ambayo hujikusanya katika bahari ya kina kifupi,” anasema Sutherland.
Mnamo mwaka wa 2017, timu ilifanya uchunguzi wa kina zaidi wa eneo hilo hadi sasa, na kuchimba zaidi ya futi 4,101 (1,250m) ndani ya bahari katika maeneo sita tofauti. Viini ambavyo walikusanya vilikuwa na chavua kutoka kwa mimea ya nchi kavu na maganda ya viumbe vilivyoishi katika bahari yenye joto na isiyo na kina.
Msokoto (halisi).
Siri nyingine inayoendelea inaweza kupatikana katika umbo la Zealandia.
“Ukiangalia ramani ya kijiolojia ya New Zealand, kuna mambo mawili ambayo yanajitokeza,” anasema Sutherland. Mojawapo mpaka unaotembea kando ya Kisiwa cha Kusini na ni muhimu sana, inaweza kuonekana kutoka katika anga.
Ya pili ni kwamba jiolojia ya New Zealand pamoja na ile ya bara hilo imepinda isiyo ya kawaida. Zote zimegawanywa mara mbili kwa mstari wa mlalo, ambapo tectonic za Pasifiki na Australia zinakutana.
Maelezo rahisi kwa hili ni kwamba sahani za tectonic zilisonga na kuharibu umbo la nje. Lakini ni jinsi gani au lini hii ilifanyika bado haijatatuliwa.
“Kuna tafsiri mbalimbali, lakini hili ni jambo kubwa lisilojulikana,” anasema Tulloch.
Sutherland anaelezea kuwa bara hilo halina mpango wa kutoa siri zake zote hivi karibuni.
“Ni vigumu sana kufanya ugunduzi, wakati kila kitu kiko kilomita 2 (maili 1.2) chini ya maji, na tabaka ambazo unahitaji sampuli ni mita 500 (1,640ft) chini ya bahari pia,” anaongeza kuwa. “Ni changamoto sana kwenda nje na kuchunguza bara kama hilo. Kwa hivyo, inachukua muda mwingi, pesa na juhudi kuchunguza maeneo.”
Ikiwa hakuna kitu kingine, bara la nane la dunia linaonyesha kwamba karibu miaka 400 baada ya jitihada za Tasman bado kuna mengi ya kugunduliwa.