Friday, November 1

RAIS Dk Hussein Mwinyi awapongeza wananchi kwa ushirikiano mkubwa ajali ya kuporomoka sehemu ya jengo la Beit al Ajaib

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo amali. Mhe Simai Mohammed Said wakati alipofika kujionea mwenyewe madhara ya kuanguka kwa jengo la Beit al Ajaib

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amefika katika eneo la Forodhani Jijini Zanzibar kwa ajili ya kuangalia ajali ya kuporomoka kwa sehemu ya jengo la Makumbusho la Taifa Beit al Ajab na kusisitiza kwamba Serikali itaendelea na juhudi za uokozi.

 

Akiwa katika eneo hilo mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa viongozi waliofika katika tukio hilo, Rais Dk. Hussein mwinyi aliwapongeza wananchi kwa mashirikiano makubwa waliyotoa.

 

Alisisitiza kwamba juhudi za uokozi zitaendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha wale wote waliofunikwa na kuta za jengo hilo wanaokolewa kwa mashirkiano ya Jeshi la Zima Moto.

 

Rais Dk. Hussein mwinyi alisisitiza kwamba Serikalin itaendelea kufuatilia na kuendelea kutoa kila ushirikiano katika kuhakikisha zoezi hilo la ukoaji linakwenda vizuri na watu wote wanaokolewa.

 

Alieleza kwamba kipaumbele kiliopo hivi sasa ni kuokoa maisha ya watu wanaosadikiwa kufunikwa na kuta za jengo hilo.

 

Juhudi kubwa zinaendelea kuchukuliwa na vikosi vya serikali katika kuhakikisha zoezi la uokozi linakwenda vizuri katika jengo hilo la Makumbusho la Taifa Beit al ajaib ambamo mnasadikiwa kwamba kulikuwa na baadhi ya mafundi ndani yake.

 

Historia zinazonesha kwamba jengo hilo ni kivutio kikuu cha utalii hapa Zanzibar kutokana na mandhari yake na historia yake hasa ikizingatiwa kwmaba katika majengo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar lililojengwa mnamo miaka ya 1883.

 

Wakati huo huo, Rais Dk. Hussein mwinyi alifika katika kambi ya huduma za macho iliyofungliwa huko katika Skuli ya Sekondari ya Mpendae, Jijini Zanzibar na kutoa shukurani kwa  uongozi wa “Bilal Muslim Mission” kwa kuamua kutoa huduma hizo kwa wananchi ambazo zitawasaidia kwa kiasi kikubwa.

 

Rais Dk. Hussein alieleza jinsi alivyofarajika na kuridhika kutokana na kiwango kikubwa cha wananchi wapatao 1200 ambao wanapatiwa huduma hizo kwa siku ambao ni watu wengi.

 

Alieleza kwamba huduma hiyo imeisaidia kwa kiasi hoapitali kuu ya Mnazi Mmoja huku akiutaka uongozi wa “Bilal Muslim Mission’  kwenda kutoa huduma zao maran kwa mara katika viswa vya Unguja na Pemba

 

Rais Dk. Mwinyi alieleza azma yake ya kuutaka uongozi wa Bilal Muslim Mission kwenda kutoa huduma hizo kisiwani Pemba .

 

Serikali kwa upande wake itaendelea kutoa mashirikiano kwa Mfuko huo wa “Bilal Muslim Mission” na kuahidi kwamba kitengo cha huduma ya macho kilichopo katika hospitakli kuu ya Rufaa ya MnaziMmoja kitaimarishwa.

 

Nae Mratibu wa huduma hizo kutoka “Bilal Muslim Mission”  Ayn Sharif alimueleza Rais Dk. Hussein kwamba huduma hizo zitatolewa kwa muda wa siku mbili katika kambi hiyo ya skuli ya Sekondari Mpendae na siku ya tatu huduma hizo  zitatolew katika hospitali Kuu ya MnaziMmoja.

 

Katika maelezo yake kiongozi huyo alimpongeza Rais Dk. Hussein Mwinyi na kueleza jinsi walivyofarajika kwa ujio wake ambao umeonesha jinsi anavyowajali wananchi wake wa Zanzibar.

 

Alieleza mashirikiano yaliopo kati yao na Madaktari kutoka hospitali kuu ya MnaziMmoja wakiwemo mataktari wataalamu wa maradhi ya macho huku akieleza azma yao ya kwenda kiswani Pemba kwa ajili ya kwenda kutoa huduma kama hizo.

 

Alisisitiza kwamba huduma zote muhimu zimekwua zikipatikana katika kambi hiyo zikiwemo dawa na kueleza kwamba kwa wale ambao wanahitaji huduma zaidi huwa wanafanya taratibu za kuwapeleka Dar-es-Salaam.

 

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822  

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk