TANGAZO
Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) inawajuilisha Walipakodi na Wananchi wote kuwa imeanza rasmi kutumia mfumo wa kutolea Risiti za Kielektroniki ujuilikanao kwa jina la Virtual Fiscal Management System (VFMS).
ZRB inawatangazia Walipakodi wote ambao wamesajiliwa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuwa hadi kufikia tarehe 01.01.2022 wanatakiwa wawe wameshaanza kutumia mashine hizo na kutoa risiti za Kielektroniki kwa wanaowauzia Bidhaa au Huduma.
Kwa tangazo hili, ZRB inawatanabahisha walipakodi wote ambao wamesajiliwa na VAT kuwa, haitaitambua Risiti yoyote ya madai (Claim) ambayo haitotolewa kwa Mashine za Kielektroniki (VFMS).
Kwa mawasiliano zaidi kuhusiana na upatikanaji wa mashine hizo, tafadhali fika ofisini kwetu Mazizini na Gombani kwa Pemba, au wasiliana nasi kupitia akaunti zetu za mitandao ya kijamii.
Aidha, ZRB inawakumbusha Walipakodi wote kuwa ni haki yao kudai Risiti kila wanapofanya manunuzi sambamba na kuwataka wafanyabiashara kutoa Risiti kila wanapofanya mauzo.
TULIPE KODI KWA MAENDELEO YA ZANZIBAR.
LIMETOLEWA NA:
KITENGO CHA UHUSIANO NA HUDUMA KWA WALIPAKODI
BODI YA MAPATO ZANZIBAR.