Monday, November 25

HABARI PICHA: Matukio mbali mbali ya uzinduzi wa miradi mbali mbali kisiwani Pemba

WAZIRI wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Dkt.Soud Nahoda Hassan (katikati), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa skuli ya Maandalizi Matangatuani Wilaya ya Micheweni, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
MBUNGE wa Jimbo la Mkoani Kisiwani Pemba Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, akikabidhi bati 150 na Mbao 450 kwa wananchi wa kijiji cha Tironi Wilaya ya Mkoani, kwa ajili ya uwezekaji wa kituo cha afya kijijini hapo
WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Lela Mohamed Mussa, ambae pia ni Kaimu waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar akikunjua kitambaa kuashiria ufunguzi wa mradi wa Umeme katika kijiji cha Mleteni, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar
WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Lela Mohamed Mussa, ambae pia ni Kaimu waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar akibonyeza kitufe kuashiria ufunguzi wa mradi wa Umeme katika kijiji cha Mleteni, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Lela Mohamed Mussa (katikati), ambae pia ni Kaimu waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar wakiangalia umeme unaowaka katika bango maalumu, baada ya kuzinduliwa katika kijiji cha mleteni, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Lela Mohamed Mussa, ambae pia ni Kaimu waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mleteni ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)