Watu watatu wakaazi wa Kangagani katika Wilaya ya Wete wamelazwa katika Hospitali ya Vitongoji Chake Chake baada ya kujeruhiwa kwa panga wakati wakiwa msikitini katika ibada ya swala ya alfajiri ya leo.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo Daktari dhamana Hospitali ya Vitongoji Dr. Sharif Khatib amesema amewapokea majeruhi hao majira ya saa kumi na mbili asubuhi na kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Juma Sadi amesema Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo .
Nae Mkuu wa Wilaya ya Wete kamanda Mohammed Mussa Mkobani amewataka wananchi wa Wilaya hio kuwa na amani huku Serikali ikishirikiana na vyombo vya sheria ili kuhakikisha muhusika wa tukio hilo anachukuliwa hatua.
Kwa upande wake Imamu wa Msikiti huo ambae pia ni sheha wa Shehia ya Kangagani ndugu Fakih Omar Yussuf pamoja na waumini wengine waliokuwepo Msikini hapo wamesema Kijana huyo alifika akiwa ameshikilia panga mkononi na ndilo alilolitumia kuwajeruhi watu hao.
Angalia video.