MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, Mtendaji mkuu wa klabu, Senzo Mazingiza pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Kilinet Mohammed Saleh na Mkuu wa bidhaa ya N-Card Khalifa Mwinyi wakisaini mkataba wa
makubaliano na Kampuni za KILINET na N-Cards kwa ajili ya kutengeneza kadi za kidigitali zitazokuwa zinatumiwa na wanachama, ikiwa ni sehemu ya hatua za awali za mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu. Kadi moja itauzwa kwa Sh. 29,000.
Yanga imeingia mkataba na kampuni za Kili- Net na N-Card kwa masuala tofauti – Kili Net – wakipewa jukumu la kusimamia na kuendesha mfumo Kidigitali, yaani kushughulikia Digital Plaoform za Yanga, usjaili wa wanachama na Social Media za klabu, wakati N-Card watafanya jukumu la kutengeneza kadi za uanachama ambazo zitawawezesha wanachama kununulia za Kielektroniki pia.