Na Talib Ussi
Mwanachama mwengine wa ACT wazalendo amechukua fomu ya Kugombea Uwenyekiti wa Taifa chama hicho huku akiahidi kuongoza chama katika misingi bora katika umoja na mshikamano.
Mwanachama huyo ambaye ni Hamad Masoud Hamad aliyaeleza hayo mara badaa ya kuomba nafasi hiyo na kukabidhiwa fomu huko katika Ofisi ya chama hicho iliyopo Mtaa wa vuga Mjini Zanzibar
Alisema ameamua kuomba nafasi hiyo kubwa kutokana na muundo mzuri uliopo katika chama hicho ambao umeleta umoja na mshikamano ambapo alifahamisha kama yeye akichaguliwa ataendeleza misingi hiyo.
Sambamba na hilo alieleza kuwa endapoatapata nafasi hiyo ataendeleza kiu ya Wazanzibar kuyapata mamlaka kamili ya serikali ya Zanzibar.
“Wazanzibar wanakiu ya kupata Zanzibar yao kuwa dola kamili kwa maana hiyo na mimi nikishapewa jukumu la uwenyekiti tutashirikiana kuongeza kasi ya kudai Zanzibar yetu” alieleza Masoud.
Alieleza kuwa amekuwa akipambana kwa maisha yake kwa siasa na kuahidi atahitimisha maisha yake akiwa ndani ya serikali inayoongozwa na chama cha ACT Wazalendo kwani ndicho kinachowatetea watu na chenye malengo ya kupata mamlaka kamili ya Zanzibar.
Hamad amesema anamini si vibaya kurithi mienendo ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho marehemu malim Seif Sharif Hamad katika kuwatetea wazanzibari ili kufikia malengo ambayo wamekusudia.
“Ni lazma tutunze miradhi siasa za maalim Seif ndizo zitakazoendelezwa ili iwe sadakatjaria na mimi nikishirikiana na wenzangu yale malengo ya kisiasa yatatimia.”alisema Hamad.
Hata hivyo alibainisha kuwa ni lazma uwepo msukumo kuhakikisha yale aliyoyawacha maalim yanaendelezwa na kutekelezwa kwa vitendo .
Hamad Masoud Hamad alizaliwa Ole mnamo Novemba 15 mwaka 1959 na alisoma shule ya msingi ole ana stashahada ya pili ya uhandisi wa ujenzi .
Hamad alifanya kazi ya ualimu kwa mika 5 na alikwenda masomoni aliporudi alifanya kazi Wizara ya maji kwa mika mitatu na akihudumu nafasi ya ukurugenzi .
Katika ulingo wa siasa Hamad alihudumu katika nafasi mbali mbali za uongozi tokea kuanzishwa kwa vyama vingi mwaka 92 hadi 2014 aliwahi kuwa Waaziri wa Mawasiliano na uchukuazi wa serikali ya Zanzibar mwaka 2010
Wanachama wa wawili wa ACT wazalendo tayari wamejitokeza kuchukuwa fomu ya Uwenyekiti na huku mmoja akichukua nafasi ya umakamu hadi leo, uchukuaji na urejeshaji fomu umeaza tarehe 4 january hadi 17 january.