Friday, March 14

ASKOFU Hafidhi ahimiza utulivu, amani na uvumilivu pemba

 

 

 

WANANCHI Kisiwani Pemba wametakiwa kuendeleza amani na utulivu iliyopo nchini, pamoja na kuvumiliana ili kufanikisha harakati zamaendeleo Serikalini.

Wito huo umetolewa na Askofu Michael  Henry Hafidh kutoka kanisa la Anglikana Zanzibar, wakati  akitoa salamu za skukuu ya Krismas kwa waumini wa dini ya Kikiristo iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Yohana Mbatiza Kizimbani Wete Pemba.

Alisema amani na utulivu ndio muhimili wa nchi katika shuhuli za kimaendeleo, hivyo wananchi wanapaswa kuitunza na kuithamini amani hiyo.

“Wazanzibari wanajivunia amani ni watu wanaoishi kwa upendo toka zamani, wanapendana, wanavumiliana ni watu wa dini, vyama, wakiristo na waislamu sio watu wakugombana bali ni wavumilivu”alisema.

Aidha aliwataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuendelea kuvumiliana, pamoja na kuwa wamoja kama alivyofanya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwanyi na Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo kuvumiliana hadi kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, baada ya kuweka uzalendo wa nchi mbele.

Alifahamisha kuwa huwezi kupelekea maendeleo sehemu yoyote kama hakuna upendo, amani, uvumilivu, hata vitambu vyote duniani vinazungumzia suala la upendo na amani.

Hata hivyo aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani, kwa uomoja wao na kuwaunganisha watu ili kuwafanya wananchi kuwa kitu kimoja.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Wete Mohamed Mussa Seif (Mkobani) alimhukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, kwa kuendelea kuhubiri suala la amani nchini pamoja na upendo na maridhiano.

Alisema katika uongozi wa Dk.Mwinyi wananchi wategemee mambo makubwa yanayokuja, huku akiwataka wakristo kusheherekea skukuu hiyo kwa amani na utulivu.

Naye kasisi Kiongozi Macon Charles Majaliwa, amesema wananchi wanapaswa kuheshimu mamlaka, tutafanyakazi kwa pamoja na bididi ili Tanzania iweze kupata maendeleo.