BAADHI ya Mdumu na Ndoo za Maji za wananchi wakijiji cha Mnarani Makangale, zikiwa kwenye foleni na kusubiri huduma ya maji inayopelekwa kwa kutumia gari la maji, kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo kwa ajili ya wananchi hao, baada ya kukosa huduma hiyo kwa muda mrefu. MKUU wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya akijaza maji katika baadhi ya ndoo za wananchi wa kijiji cha mnarani Makangale, kufuatia wananchi hao kukosa huduma hiyo kwa muda mrefu na kulazimika kuwapelekea gari la maji kila muda ili waweze kupata huduma hiyo. MDHAMINI wa Kamisheni ya Utalii Pemba Hamad Amini Ali, akizungumza na wanafunzi wa skuli ya Madungu Sekondari, baada ya kufanya usafi katika fukwe ya Shamiani Mwambe, kwa lengo la kutangaza fukwe hiyo kuwa kivutio cha utalii ndani ya kisiwa cha Pemba. BAADHI ya wanafunzi wa skuli ya Madungu Sekondari wakifanya usafi katika Ufukwe wa Kisiwa cha Shamiani Mwambe, ikiwa ni lengo la kuutangaza Ufukwe huo kuwa kivutio cha utalii Pemba WANAFUNZI wa Skuli ya Madungu Sekondari wakizoa taka baada ya kufanya usafi katika ufukwe wa Kisiwa cha Shamiani Mwambe, ikiwa ni mikakati ya kutangaza ufukwe huo kuwa kivutio cha Utalii Pemba MIONGONI mwa Fukwe bora, kubwa na safi Kisiwani Pemba kwa sasa ni Ufukwe wa Kisiwa cha Shamiani Mwambe, ikiwa ni moja ya vivutio vikubwa vya utalii ndani ya Kisiwa cha Pemba (PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) Share