Monday, November 25

Skuli ya Msingi Mchangamoto yaondokana na kadhia ya maji safi na salama.

NA ABDI SULEIMAN.
MBUNGE wa Jimbo la Kojani Hamad Hassan Chande, amesema kuzinduliwa kwa mradi wa maji safi na salama katika skuli ya Msingi Mchangamoto, utaweza kuwaondoshea shida wanafunzi wa juu upatikanaji wa huduma hiyo nje ya skuli.
Alisema kwa sasa wanafunzi wa skuli hiyo hatosumbuka tena katika suala la uhitaji wa maji, kwani maji watayapata ndani ya skuli yao na haitokua na haja ya kutoka nje.
Mbunge Chande pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, aliyaeleza hayo katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa huo wa maji safi na salama, uliojengwa kupitia ufadhili wa Rehema Foundation.
Alisema uwepo wa mradi huo wa maji utaweza kluwafanya wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao, kwani suala la amaji lina umuhimu mkubwa hususana kwa wanafunzi.
“Hapa wanafunzi walikuwa wakisumbuka wakati wanapotaka kujisaidia, wakati mwengine vyoo vinakosa maji jambo ambalo hatari kwao, sasa maji hayo yatawasaidia sana hata kuokoa afya zao,”alisema.
Aidha mbunge huyo aliahidi kuendelea kusaidia kwa hali na mali changamoto zozozte zitakazotokea katika skuli hizo, kwa lengo la kuwafanya wanafunzi kupata elimu bora.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshuhulikia watu wenye ulemavu Ummy Nderiannga, alisema wananchi wa Kojani wamepata mtu sahihi wakutatua matatizo yao ndani ya Jimbo.
Naibu huyo aliipongeza taasisi ya Rehema Foundation na mbunge huyo, kwa kutatua tatizo la maji katika skuli hiyo ikizingatiwa skuli ina wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Aidha aliwataka walimu wa skuli hiyo, kuhakikisha wanawapatia elimu ipasavyo na kuwaangalia wanafunzi wenye ulemavu, ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
“Hii skuli imenivutia sana nimeona kuwa ni moja ya skuli muhimu sana kwetu, vijana hawa licha ya ulemavu wao nao wanahaki ya kupata elimu kama ilivyo wanafunzi wengine,”alisema.
Mwakilishi wa Rehema Foundation Mohamed Asaa, aliwataka walimu, wanafunzi wa skuli ya Mchangamdogo Msingi, kuhakikisha wanautunza na mradi wa maji safi na salama skulini hapo.
Alisema kudumu kwa muda mrefu kwa mradi huo utaweza kuifanya taasisi hiyo, kuwapatia mradi mwengine kwa lengo la kupunguza changamoto zinazoikabili skuli hiyo.
Naye mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi Mchanga mdogo Suleiman Khatib Kombo, alisema kuzinduliwa kwa mradi huo wa maji safi utaondosha tataizo la maji katika skuli hiyo.
“Tulikuwa nayo maji ya ZAWA lakini yamekatika hafla katika skuli yetu, tulifuatilia lakini hatukupata jibu, sasa tunashukuru kwa viongozi waliotupatia mradio huo”alisema.
Kwa upande wao wanafunzi wa skuli hiyo, wamempongeza mbunge huyo kwa kuwatatuli kilio cha maji katika skuli yao, kwani walikuw awakisumbuka wakati wanapohitaji kwenda kujisaidia.