NA ABDI SULEIMAN.
AFISA Usajili ardhi na utoaji wa hati miliki kutoka Kamisheni ya Ardhi Pemba Yussuf Hamad Kombo, amesema ili kuweza kupunguza migogoro ya ardhi katika jamii na wanawake kupata haki zao kisheria.
Alisema ardhi ni rasilimali pekee ambayo inamsaidia mtu baada ya kuisajili kisheria, kwani anamuondoshea matatizo mbali mbali ikiwemo kuepusha na migogoro.
Afisa huyo aliyaeleza hayo mjini chake chake, katika mkutano wasiku moja ulioyashirikisha mabaraza ya ardhi ya wanawake Mkoa wa kusini Pemba, kupitia mradi wa uhamasiahaji wa upatikanaji wa haki za usimamizi wa ardhi kwa wanawake, unaotekelezwa na jumuiya ya PECEO kwa ufadhili wa FCS.
Alisema kamisheni ya ardhi inaongozwa na sheria saba (7)zote zinahakikisha ardhi ardhi inakuwa salama na serikali ndio mmiliki wa ardhi.
Alifahamisha kuwa lengo la sheria hizo ni kuondosha migogoro ya ardhi katika jamii, kwani ardhi ni nyenzo muhimu katika ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja moja au kikundi.
Aidha alizitaja sheria hizo kua ni sheria ya kamisheni ya ardhi NO:6 ya mwaka 2015, sheria ya utambuzi wa ardhi NO:8 ya mwaka 1990, sheria ya upimaji NO:9 ya mwaka 1990, sheria ya usajili wa ardhi NO:10 mwaka 1990.
Sheria nyengine ni sheria ya umiliki wa ardhi NO:12 ya mwaka 1992, sheria ya Mahakama ya ardhi NO:7 ya mwaka 1994 na sheria ya uhaulishaji ardhi NO:8 ya mwaka 1994.
“Kwa sasa serikali iko katika mipango ya kutambua maeneo yote, kupimwa na kupatiwa hati yake, tulimeanza na shehia 10 kwa sasa, ila hadi sasa hati 900 zimetayarishwa na hati 260 zimeshaenda kwa wenyewe”alisema.
Mratib wa Jumuiya zisizo za kiserikali Pemba Ashrak Hamad Ali, aliwasisitiwashiriki hao kuwa wanapomiliki ardhi kuwa na vielelezo kutoka serikali ili waweze kuzitumia wanapofikwa na matataizo.
Alisema kuna mizozo mingi sana ya ardhi kwa sababubu umiliki hauna vielelezo, umiliki ambao hauwezi kumsaidia mtu pale anapopatwa na taatizo.
Aidha alisema mabaraza ya ardhi ya wanawake, yanaumuhimu mkubwa sana wa kuelimisha jamii kusuhisiana na suala zima la kutoa elimu, hasa kwa wanawake walioko pembezoni.
“PECEO munapaswa kuendelea kuomba mradi mwengine na usiwe mradi wa mkoa au wilaya, bali uwe mradi wa Pemba nzima kwani matatizo ya ardhi yapo mengine na wanawake ndio waathirika wakubwa”alisema.
Katibu wa PECEO Juma Saidi Ali, alisema sababu kubwa ni wanawake kukosa uwelewa juu ya suala la umiliki wa ardhi, hawajuwi haki zao za msingi mafunzo hayo yataweza kuwafanya kujuwa mambo mengi katika masuala ya ardhi.
Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Chake Chake Stara Khamis Juma, alisema wanawake ni wahanga wakubwa katika matatizo ya ardhi, hivyo wanapawa kuitumia nafasi hiyo katika kupata haki zao za ardhi.
Nao baadhi ya wanawake wamesema mwanamke anapomiliki ardhi anaepukana kuwa na utegemezi kwa mwenzake wake, hivyo wanapasawa kuwa makini katika kufuata sheria.
MWISHO