Monday, November 25

Waziri lela akabidhi mabanda mawili yenye madarasa matano ya kusomea skuli ya Chambani Msingi.

NA ABDI SULEIMAN.

Mwakilishi wa Viti maalumu UWT wasomi Mkoa wa Kusini Pemba, Lela Mohamed Mussa, amekabidhi mabanda mawili yenye madarasa matano ya kusomea wanafunzi kwa uongozi wa skuli ya Chambani Msingi.

Vyumba hivyo vimekabidhiwa kwa uongozi huo baada ya kufanyiwa matengenezo makubwa ya ujenzi wake, ili viweze kuendana na mazingira hali ya wanafunzi kupata elimu iliyobora.

akizungumza katika mkutano wa kukabidhi vyumba hivyo uliowakutanisha walimu, wanafuni na kamati ya skuli ya msingi na sekondari Chambani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.

Waziri Lela alisema madarasa hayo yalikuwa katika hali mbaya, licha ya skuli hiyo kuwa kongwe na yazamani sana lakini wajibu wake ni kusaidia maendeleo ya mkoa huo.

Aidha aliwataka wanafunzi na walimu kubadilika na kuondokana na dhana potofu katika suala zima la elimu, kwani malengo ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ni kuhimiza maendeleo.

“Leo hapa sote ni mashahidi katika hafla hii, hivi vyumba mapaka kumalizika kwakwe vimegharimu Milioni 1,500,000/=, huku akiwasihi walimu wa chambani kupunguza migogoro baina yao na wanafunzi.

Aliwasihi walimu kutambua kuwa wanadhima kubwa katika kuwafunidha watoto elimu bora, licha ya changamoto wanazokumbana na zo katika kuona wanafunzi wanapata haki yao ya kikatiba.

Kwa upande wake Mwwenyekiti wa kamati ya skuli Nassor Suleiman Nassor, alimshukuru mwakilishi huyo kwa juhudi zake alizozichukua kuhakikisha wanafunzi wanapata mabanda mazuri kulinga na elimu wanayopatiwa.

Alisema skuli hiyo ni miongoni mwa skuli konge ilianzishwa 1947 ikiwa na wanafunzi 26, sasa imekua na wanafunzi 1521 wanawkae 770 na wanaume 713 na walimu 17.

Aidha mwalimu huyo aliahidi kuhakikisha mambanda hayo yanatunzwa na kulindwa, ili kuweza kudumu kwa muda mrefu kwani bado wanahitaji tena na mabanda mengine mapya ya kusomea wanafunzi.

Nao baadhi ya wanafunzi wa skuli hiyo, wamempongeza mwakilishi huyo kwa juhudi zake alizozichukua za kuwafanyia ukarabati majengo hayo.