Monday, November 25

MAKALA:Uvunjifu wa amani unaofanywa na vijana hautokani na malezi -Wazazi, walezi wadai mitandao ya kijamii, wanasiasa ndio chanzo

NA MARYAM SALUM, PEMBA
SUALA la malezi ya vijana, ni moja ya jukumu kubwa lisiloepukika kwa wazazi.
Hapa hasa lengo ni kuona malezi wanayotoa yanaendana na misingi na maadili, yatakayowasaidia kujitenganisha kwenye vikundi hatarishi ambavyo mwisho wa siku ni uvunjifu wa amani nchini.
Kila mzazi anawajibu mkubwa kuwapa maelezi bora wale wanao wamiliki katika familia, ikiwemo kuwahimiza katika kutenda mambo mema.
Kwa wazazi kuwalea watoto (vijana ), katika kuwahimiza mambo kadhaa mema likiwemo la kudumisha amani, ambayo ni moja ya hazina kubwa.
Amapo hazina hii Muumba, ameiweka amani na sasa kila mmoja na kwa nafasi yake hutakiwa kuilinda na kuidumisha wakati wote.
NINI MAANA YA AMANI
NI mchakato wa kuishi bila guguza, makero, kejeli, dharau ili hapo sasa kila mmoja aishi kwa utulivu, hali ambayo itamfanya kuishi bila ya tatizo lolote na kuweza kufanya shughuli zake bila ya kuingiliwa.
Vijana waliowengi wamekuwa wakiiga mambo ya nje kama vile mavazi, mikato ya nywele, uvaaji nguo, lakini pia wamekuwa wakipokea ushawishi kutoka kwa watu fulani kwa ajili ya uvunjaji wa amani.
Mkuu wa Wilaya ya Wete Hamad Omar Bakar alisema Serikali inawajibu wa kuhimiza amani wakati wowote bila ya kujali ni wakati gani.
Dc Omar anasema vijana wamekuwa wakihimizwa kudumisha amani na kupewa ushahidi wa nchi jirani zilivyokosa amani na zilivyosasa.
“ Hakuna nchi yoyote inayoweza kuendelea kiuchumi na ustawi wa jamii bila ya kuwa na amani, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kutokubali vishawishiwa kuvuruga amani yao,”alieleza.
WAZAZI NA MALEZI YA VIJANA
Shara Nassor Ali (55), mkaazi wa Masota shehia ya Shengejuu, wilaya ya Wete, anasema suala la malezi na makuzi ya vijana litaendelea kuwa la mzazi mwenyewe, huku akiwatenganisha na uvunjifu wa amani.
“Wazazi tumekuwa tukiwapatia vijana wetu malezi bora yenye heshima, lakini vijana kuonekana kuiga baadhi ya mambo na kujikita zaidi kwenye mitandao isiyokuwa na maslahi kwao,’’anafafanua.
jambo ambalo linapelekea kuwepo kwa matukio mengi ya uvunjifu wa amani,”alisema.
Aliwataka wazazi wenzake kuwalea vijana wao katika kudumisha amani ya nchi, na kuwakataza kutojiingiza katika matendo ya uvunjifu wa amani ambayo ikitoweka ni gharama kubwa kuirejesha.
Fatma Abdalla Kombo (40) mkaazi wa Chwale Wete anaona kuwa malezi yaliyopo kwa vijana yanasaidia kwa njia moja ama nyengine kuona wanajiepusha na suala la uvunjifu wa amani nchini.
“Hakika hakuna mzazi asiyemlea mwanawe malezi mazuri, isipokuwa vijana wenyewe wanajiona wamewahi wanajua kutumia mitandao watakavyo bila kuulizwa na mtu, hapo ndipo vijana wengi kuonekana kupotoka na kusahau malezi wanayopewa,” alisema Fatma.
“Niseme tu malezi yapo lakini kumekuwa na utofauti wa malezi ya sasa na ya zamani, kwani wazazi walikuwa na malezi ya pamoja katika kulea vijana wao, lakini sasa hayapo,’’anabainisha.
Aliwataka wazazi waondokane na malezi ya mtu pekee, washirikiane kwenye malezi ili vijana waondokane na masuala mbali mbali ikiwemo ya uvunjifu wa amani.
Saidi Mussa Rashid ambae ni Mwenyekiti wa Jumuia ya vijana wilaya ya Wete, (PYVO) alieleza vijana wamekuwa wakipewa malezi yakutosha, lakini ipo haja kuongezewa elimu juu ya kudumisha amani.
Alisema wazazi wawe na utamaduni wa kukaa na vijana wao kuwaelezea umuhimu wa kudumisha amani na hatari ya kuvunjika kwake.
Anaeleza kuwa, kwa upande wa jumuiya imekuwa ikitowa mafunzo hayo pale wanapokutana nao, ingawa anaona haitoshi iwapo wazazi watakuwa kimya.
“Ili tufikie lengo basi wazazi nao wapewe elimu juu ya umuhimu wa kurejesha malezi ya pamoja kama ilivyokuwa zamani,ili kuwa na vija wenye maendeleo,”alieleza.
Ali Hamdi Ali (35) Mchangamdogo alieleza kuwa malezi yanayotolewa yanasaidia vijana kujitenganisha na uvunjifu wa amani, lakini kinachorejesha nyuma ni kutokana na baadhi ya wazazi kua na tabia ya kusema kila mtu na mwanawe.
Hivyo ili vijana waepukane kutumika kwenye mambo ya uvunjifu wa mani, ni vyema wazazi kushirikiana katika malezi ili wafikie malengo.
“Lakini kinachopelekea vijana kujiingiza kwenye uvunjifu wa amani ni kutokana na tamaa kwenye nafsi zao bila kujua athari zinazoweza kuwapata,”anabainisha.
Hamad Saleh Ali (30) mkaazi wa Likoni Wete, alifahamisha kuwa malezi kwa vijana yana umuhimu mkubwa, lengo ni kujiepusha na masuala mbali mbali ya uvunjifu wa amani nchini.
“Endapo wazazi watajenga umoja kwenye malezi kwa vijana wao kwakushirikiana na jamii nyengine basi vijana wataepukana kujiingiza katika uvunjifu wa amani,”.
Rukia Ibrahim (30) anasema hakuna hata kijana mmoja kwenye malezi yake anaelekezwa kuichafua amani, ila yapo makundi kama ya wanasiasa wanakuwa ndio adui wa vijana.
“Vijana wakiambiwa waingie barabarani hukubali bila ya kujali athari, na kusahau kuwa wamelelewa kimaadili na malezi yanayowatenganisha na uvunjifu wa amani,’’anasema,
Lakini hata Sada Saleh Ali (32) anasema suala la uvunjifu wa amani walilonalo baadhi ya vijana, hutokana na ushawishi wa makundi kama ya wanasiasa. #FCS
“Malezi tunayopewa hayana uhusiano na uvunjifu wa amani, bali ni sisi tu baadhi yetu kichwa ngumu,’’anabainisha kijana Saada.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Richard Tadei Mchomvu alieleza kuwa ni vyema vijana kutokubali kuwa ni watu wakutumiliwa kuvunja amani. European Union in Tanzania
“Lakini tu kutokana na vijana wenyewe kujikita zaidi kwenye utandawazi na kujiona wamefika, husahau malezi wanayopewa na wazazi wao, na kujiingiza kwenye matukio mbali mbali yakiwemo ya uvunjifu wa amani,”alisema.
Jeshi la Polisi limejipanga kuona wanatoa elimu kwa jamii katika kuwalea vijana wao kwenye malezi yenye maadili, ili waepukane kujiingiza kwenye uvunjifu wa amani kwani kuna adhabu juu ya uvunjaji wa amani. Search for Common Ground Tanzania
Aliwataka vijana wasijisahau kwenye maisha watumie malezi na maadili wanayopewa na jamii ili kujiepusha kuwa chanzo cha uvunjivu wa amani.
Sheikh Said Ahmad Mohamed kutoka Ofisi ya mufti Pemba, alieleza kuwa suala la malezi bora kwa vijana, linasaidia kwa asilimia 90, katika kuwatenganisha na uvunjifu wa amani.
Alisema wamekuwa wakiona wazazi jinsi wanavyojitahidi kuwapatia malezi vijana wao ili waepukane na mambo mbali mbali yakiwemo ya uvunjifu wa amani.
“Walatuswaghiru swadaka linnasi wala tamshi fil-ardh maragha, usiwaangalie watu kwa jicho la jeuri na wala usitembee katika ardhi kwa maringo kwani mwenyezi Mungu hawapendi wale wenye kiburi wajivunao,”.
Akatoa mfano kuwa, Lukumani wakati akimpa malezi kijana wake alimwambia ‘ewe mtoto wangu hakika ikiwa jambo utakalolifanya lenye ukubwa sawasawa na mdudu chungu na jambo hilo ukalifanya kwa uficho, basi mwenyezimungu siku ya kiama ataleta litabainika.
Nae mchungaji wa Kanisa la Walokole liliopo Makangale Elius Maganga alieleza kuwa malezi wanayopewa vijana yananafasi kubwa juu ya kujitenganisha na uvunjfu wa amani.
“ Bibilia inasema, “tafuteni kwa bidii kuwa na watu wote, na huo utakatifu ambao munao iwapo mutaoondosha hapana mtu atakae muona Mungu” , Mchungaji Maganga alisema.
Alifahamisha ili kuhakikisha utakatifu ni kutenda mema ili utawale vizuri na uwe na maamuzi yasio na shaka , uwepo wa amani ni furaha kwa jamii na taifa, kitabu cha Waibrania mlango wa 12 msitari wa 14 inaeleza hivyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tumaini Jipya Pemba ‘TUJIPE’ Tatu Abdalla Msellemu, alieleza kumekuwa na utofauti mkubwa kati ya malezi ya sasa na ya zamani kwa vijana. Pemba Pressclub
Kwa maoni yake anaona kuwa, malezi yaliyopo sasa hayatoshi kutokana na wazazi wenyewe kusahau majukumu yao katika malezi kwa kizazi cha sasa.
“Malezi wanayolelewa vijana wa sasa imekuwa chanzo kusahau malezi na maadili waliyolelewa, na badala yake kuiga mambo yasiyofaa ikiwemo uvunjifu wa amani,”anafafanua. Dr. Hussein Ali Mwinyi
Afisa Mdhamini Wizara ya Habari vijana Sanaa Utamaduni na Michezo Pemba Salim Ubwa Nassor, alisema malezi yapo, lakini kutokana na vijana kutojielewa imekuwa chanzo kutumiwa na watu wabaya katika uchafuzi wa amani. Internews in Tanzania
“Moja tunalolifanya nikuwapatia malezi vijana, kuwaweka pamoja kwa kutumia mabaraza ya vijana bila ya kujali tofauti za kisiasa ili kuona wanajitenganisha na uvunjifu wa amani nchini,” alisema.
Alifahamisha kuwa licha ya malezi wanayopewa kwa wazazi wao, huwapatia mafunzo mbali mbali ya uzalendo, uadilifu na uwajibikaji ambapo ndani yake hupata mafunzo ya kudumisha amani.
Mwinyi Juma Hamad Mkurugenzi wa haki za binaadam na utawala bora wa chama cha siasa cha ACT, Mkoa wa kaskazini Pemba, anasema wamekuwa wakihubiri suala la amani, na kuwataka vijana wafuate malezi, wanayopatiwa katika kulinda amani. Uhuru Gazeti
Aliwataka vijana kuhakikisha wanasimamia kulinda amani, kwani bila amani hakuna utawala, hakuna watakalofanya likafanikiwa. #pembatoday
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Khamis Dadi Khamis, alieleza kama ilivyosera ya Chama cha Mapinduzi inaendelea kuhubiri suala zima la amani nchini.
“Hivyo kama viongozi wa vyama tunajukumu kubwa la kutoa malezi kwa vijana kuhakikisha wanajitenganisha katika uvunjifu wa amani,” alisema. Utpc TZ
Msaidizi Afisa miradi kutoka taasisi ya Search for Common Ground Pemba Khamis Abas Khamis alisema kuwa wamekuwa wakiyawezesha makundi mbali mbali ndani ya jamii ili kuyapa elimu ya utatuzi wa migogo,” alisema.
“Hata klabu ya wandishi wa habari Pemba Press klab PPC, inayomradi wa miezi sita (6) moja ya malengo hayo ni kuwawezesha waandishi wa habari kuandika habari za utatuzi wa migogoro na kudumisha amani. #PPC
Akizindua mradi wa Mani yangu Sauti yangu Khatma yangu mwenyekiti wa PPC Bakari Mussa Juma amesema kalamu ya waandishi wa habari ikitumika vyema inaweza kuwa chanzo cha kuepusha mifarakano. Pemba Today
“Kundi kama la vijana lisipozingatia malkezi ya famila zao na kujirahisisha kwa wanasiasa wanaweza kuwa msingi mzuri wa uchafuzi w amani,” alisema mwenyekiti huyo.
MWISHO.