Sunday, November 24

HABARI PICHA: WATENDAJI wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wafanya usafi Fukwe ya Vumawimbi.

MKUU wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahaya, akizoa taka na kutia katika bero wakati wa zoezi la usafishaji wa Fukwe ya Vumawimbi, iliyopo kijiji cha Makangale Wilaya ya Micheweni ikiwa utangazaji wa Ufukwe huo kwa watalii
WATENDAJI wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Abdalla Rashid na Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete Salma Abouu Hamad, wakifagia ufukwe wa Vumawimbi ikiwa ni ishara ya zoezi la ufanyaji usafi katika fukwe hiyo
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mattar Zahor Masoud (kushoto) akifukiwa takataka katika moja ya shimo walilolichimba, wakati wa zoezi la ufanyaji usafi ufukwe wa Vumawimbi, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali na Mkuu wa Wilaya ya Wete Mgeni Khatib Yahya
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Matar Zahor Masoud, (katikati) akiwaongoza viongozi mbali mbali wa serikali katika kusafisha ufukwe wa Vumawimbi Wilaya ya Micheweni, ikiwa ni Zoezi la Kufanya usafi katika fukwe hiyo iliyoko Micheweni
MKUU wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya akimimina taka katika bero kwa ajili ya kwenda kutupwa sehemu maalumu, wakati wa zoezi la ufanyaji usafi katika Fukwe ya Vumawimbi Wilaya ya Micheweni

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)