Monday, November 25

SABABU NANE ZILIZOFANYA GSM KUVUNJA MKATABA NA TFF

1. Mechi zote za nyumbani zinazoihusisha Simba zimekuwa zikichezwa bila ya nembo ya GSM kwenye mbao za matangazo hii ni kinyume na kifungu namba 4.1 na 4.8 cha makubaliano ya udhamini.

 

2. GSM kwa makusudi imenyimwa haki ya kuonekana kwenye bango la mandhari la wadhamini kwa mikutano yote inayohusishwa Simba hii ni kinyume na kifungu namba 4.8 cha makubaliano ya mkataba.

 

3. GSM kwa makusidi imenyimwa haki ya kuonekana kwenye mabango ya mikutano ya kabla na baada ya mechi mwenyeji mechi zinazoihusisha Simba.

 

4. GSM kwa makusudi imenyimwa haki ya kuonekana kwenye bega la kushoto la jezi za Simba.

 

5. TFF wameshindwa kujibu juu ya malalamiko yetu na kushindwa kurekebisha ukiukwaji wa makubaliano kama tulivyowasilisha taarifa ya ukiukwaji tarehe 14 Disemba 2021.

 

6. TFF imeshindwa kutimiza kanuni zake juu ya wadhamini.

 

7. Nembo za GSM na Chapa yake zimekua hazieshimiwi na maafisa wa TFF mara kwa mara.

 

8. TFF imeshindwa kuweka usawa kwenye mechi za ligi kuu.