NA ABDI SULEIMAN.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, amewataka wazazi wa Jimbo la Kiwani kuzudisha juhudi katika kuwasimamia watoto kwenyen suala la elimu, kwani bila ya elimu hakuna maendeleo yoyote yatakayofikiwa.
Alisema iwapo wanafunzi watasimamiwa ipasavyo katika masomo yao na kupata elimu bora, basi wataalamu mbali mbali wakiwemo Walimu, madaktari, injinia, wahasibu wataweza kupatikana.
Makamu aliyaeleza hayo alipokua akizungumza na wananchi wa Kiwani, kupitia simu ya Mkononi ya Mbunge wa Jimbo hilo wakati wa sherehe maalumu ya makabidhiano ya jengo lenye madarasa matatu ya kusomea, lililojengwa na Makamu huyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa kwa skuli ya Kiwani alipokua Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.
Alisema wazazi, walimu, na viongozi wa jimbo hilo, wanapaswa kushirikiana katika kuleta maendeleo ya elimu ndani ya jimbo hilo, kwani mikakati walioiweka imeanza kuzaa matunda kwa kutoa michipuo na vipawa wanafunzi 20 kwa hatia ya kwanza.
“Nimefarajika sana kuona leo imefika siku ya kukabidhiwa madarasa hayo, nipotayari kushirikiana kwa lolote ili kuona mafanikio yanafikiwa,”alisema.
Aidha aliwataka wananchi kutambua kuwa katika fedha za COVID 19, skuli ya msingi Kiwiani itapata matundu matano ya vyoo na Skuli ya Msingi Tasini kujengewa matundu sita ya vyoo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, alisema suala la elimu linaumuhimu mkubwa sana kwa jamii, ndio maana serikali ya awamu ya nane imedhamiria kujenga skuli za kisasa katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.
Alisema uwepo wa miundombinu mizuri inawafanya hata wanafunzi kuhamasika kusoma, hivyo serikali hiyo imeona ipo haja ya kuondosha tataizo la uhaba wa madarasa nchini.
“Kuwepo kwa skuli ya msingi na Sekondari hapa Kiwani, pamoja na dahalia la wanafunzikutaongeza chachu ya ufaulu kwa vijana,”alisema.
Aidha aliwataka walimu kujitoa kwa moyo wao, kutumia mbinu, weledi ili kuhakikisha wanapasisha wanafunzi wengi, sambamba na wazazi kuchukua jukumu la kupitia mabuku ya watoto wao wanaporudi majumbani.
Mbunge wa jimbo la Kiwani Rashid Abdalla Rashid, aliwataka walimu na wanafunzi kuhakikisha wanayataumia madarasa hayo ya kisasa kwa ajili ya kupata matokeo mazuri ya wanafunzi.
Aidha aliwahidi wanafunzi, walimu na wasimamizi wa kambi ya mbunge, kwamba mwaka huu kambi itaanza mapama na hakutakua na shida ya kutafuta sehemu kwani dakhalia litakua limeshakamilika.
Naye Mwakilishi wa jimbo hilo Fumu Mussa Fumu, aliwataka wananchi kushirikiana katika suala la maendeleo ya jimbo lao, kwani maendeleo aliyofanya makamu wa Pili kwa wananchi wa Kiwani ni mambo makubwa.
Kaimu Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mapunzo ya Amali Pemba, Mwalimu Harith Bakar Waziri, alimuomba Makamu wa Pili kuwapatia jengo la ghorofa katika skuli ya Kiwani kwani nafasi ya ujenzi huo upo.
Akisoma risala Mwalimu Khamis Ali Khalfani, alisema ujenzi wa Jengo moja lenye vumba vitatu vya kusomea, Meza na viti vyake vyote vimegharimu Jumla ya shilingi Milioni 43,407,000/= tayari ujenzi umeshakamilika kwa asilimia 100%.
Alisema changamoto kubwa kwa sasa, skuli hiyo ina wanafunzi 1458, wanafunzi 777 ni wavulana wanahitaji matundu 17 ya vyoo kwa wastani wa tundu moja wanafunzi 45 na wanafunzi 681 ni wanawake wanaohitaji matundu 17 wastani wa tundu wanafunzi 40 kwa sasa skuli ikiwa na maqtundi 10 na upund=gufu wa matundi 24.