
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Ligi ya Mabingwa Ulaya inarejea tena wiki hii ambapo Paris St-Germain inakutana na Real Madrid na Sporting Lisbon inawakaribisha Manchester City usiku wa siku ya Jumanne.
Wakati ligi hii ghali tukurejeshe kwenye mambo muhimu yakuyaangalia huku tukikukumbusha timu gani zimetolewa na timu gani zinaendelea na safari ya kuwania kombe la michuano hili, linaloshikiliwa na Chelsea kwa sasa.
Ulaya bila Barcelona

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 18 kwa Barcelona kutotinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Gazeti la Uhispania la AS liliitaja kuwa ni “kuporomoka kwa Barcelona kutoka kundi la wababe wa soka” wakati walipochapwa 3-0 dhidi ya Bayern Munich na kumaliza katika nafasi ya tatu (kilikuwa kipigo cha 3-0 cha tatu katika michezo yao sita).
Badala ya kushindana kwenye michuano hii mikubwa na ya kifahari zaidi kwa ngazi ya klabu, watakuwa wakikabiliana na Napoli (ambao walimaliza juu ya Leicester) katika mchezo wa 16 bora ya michuano dada ya Europa League.
Timu za England kiulaini.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
- Sporting Lisbon v Manchester City
- Chelsea v Lille
- Atletico Madrid v Manchester United
- Inter Milan v Liverpool
Hii ni mara ya nne katika misimu mitano angalau timu nne za England zinafuzu kwenye 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya- zote zikifuzu huku zikiwa na mchezo mmoja mkononi.
Timu tatu katika hizo ni miongoni mwa timu nne zinazopigiwa chapuo kutwaa ubingwa wa michuano hii (Manchester City, Bayern Munich, Liverpool na Chelsea).
Timu zote za Uingereza zinakabiliana na mabingwa wa ndani wa ligi nne kati ya tano za Ulaya (Hispania, Italia, Ufaransa, Ureno).
Timu zote za Uingereza zinakutana na mabingwa wa ndani wa ligi nne kati ya tano za Ulaya (Hispania, Italia, Ufaransa, Ureno).
Hata hivyo, katika mabingwa hao hakuna hata timu moja inayoongoza ligi kwa sasa.
Msimu uliopita Chelsea iliichapa City katika fainali – inaweza kuwa hadithi kama hiyo mwaka huu? Pep Guardiola anaweza kutwaa taji hilo bila ya Barcelona na Lionel Messi?
Timu mchanganyiko

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Timu 16 zilizofuzu hatua hii ya 16bora zinatoka katika ligi nane tofauti – ikiwa ni pamoja na Red Bull Salzburg aliyeingia hatua hiyo kwa mara ya kwanza.
Salzburg, Ajax, Benfica na Sporting Lisbon inamaanisha kuwa kuna timu nyingi kutoka nje ya ligi tano bora za Ulaya kuliko miaka mitatu iliyopita kwa pamoja (Porto mwaka 2021 na 2019 na Ajax mwaka 2019).
Ajax – ambayo ni ya pili kwa kufumania nyavu katika ligi ya mabingwa msimu huu ikiwa na mabao 20 – na Sporting zimefuzu kutoka kundi moja lililokuwa na Borussia Dortmund.
Kunaweza kuwa na mfungaji bora mpya pia wa michuano ya msimu huu, huku Sebastien Haller wa Ajax akiongoza akiwa na mabao 10 (katika michezo sita tu) na Christopher Nkunku wa RB Leipzig akiwa wa tatu kwa mabao saba.
Nani kunufaika na kurejewa kwa droo ya ratiba?
Droo ya michezo hii ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilipaswa kufanyika mara mbili baada ya makosa kufanyika katika drooya awali.
Awali kabla ya matatizo ya kiufundi ya upangaji ratiba kubainika Manchester United ilipangwa kukutana na moja ya timu zinazopigiwa upatu, Paris St-Germain – Cristiano Ronaldo v Messi.
Sasa watakutana na Atletico Madrid, ambao wako nje ya nne bora katika La Liga. PSG ambayo pengine ingependelea droo ya kwanza waliopangwa kukutana na United, sasa wamepelekwa mikononi mwa Real Madrid.
Liverpool iliyokuwa ikutane awali na mpinzani mtata klabu ya Austria ya Red Bull Salzburg sasa inakipiga na mabingwa wa Serie A na vinara kwa sasa wa ligi hiyo ya Italia, Inter Milan.
Manchester City itacheza na Sporting Lisbon badala ya Villarreal, wakati Chelsea ilipangwa na Lille mara zote mbili.
Timu ambayo inakutana na mtihani mzito kwenye ratiba mpya ni Bayern Munich, ambao walipangwa kukipiga na Atletico Madrid sasa wanakutana na Salzburg. Real Madrid waliokuwa wakutane na Benfica, sasa watakipiga na PSG.
Hakuna goli la ugenini

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Kwa mara ya kwanza hatua za mtoano za Ligi ya Mabingwa Ulaya hakutakuwa na faida ya goli la ugenini tangu Uefa ilipofuta kanuni ya magoli ya ugenini.
Timu zikilingana na mabao katika mizunguko ote miwili , basi utaongezwa muda na baadae kama zimetoka sare , mikwaju ya penati itaamua atakayesonga mbele.
Inaweza kuondoa ladha na msisimko wa michezo ya mtoano. Ushindi maarufu wa Tottenham dhidi ya Ajax na Manchester City kwenye michuano hii, kwa sheria hii mpya, mechi hizo zingeenda muda wa ziada wa dakika 30.
Hivyo hivyo kwa ushindi wa United dhidi ya PSG ambao ulimsaidia Ole Gunnar Solskjaer kupata kazi ya umeneja, na ule mchezo wa Roma dhidi ya Barcelona.
Messi ataweza kuipa Ubingwa wa kwanza PSG?

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Wakati PSG ilipomsajili Messi, haikuwa kuwasaidia kurejesha taji la Ligue 1 – lengo ilikuwa ni ili waweze kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya.
PSG bado haijashinda ligi ya mabingwa katika muongo mmoja wa umiliki wa Qatar na uwekezaji mkubwa uliofanywa, mwaka 2020 ilichapwa na Bayern Munich katika mchezo wa fainali.
Wana washambuliaji watatu bora katika soka la dunia – Messi, Neymar na Kylian Mbappe.
PSG ilikataa ofa ya £137m kutoka Real Madrid kwa ajili ya Mbappe katika dirisha la usajili la majira ya joto msimu uliopita licha ya ukweli kwamba anaweza kuondoka kwa uhamisho wa bure mwezi Julai – hivyo huu unaweza kuwa msimu pekee walionao wakiwa na washambuliaji hao watatu kwa pamoja.
Pamoja na Messi kufikisha umri wa miaka 35 mwishoni mwa msimu huu, inaweza kuwa fursa nzuri kwa pande zote mbili, huku Messi akiwa na matumaini ya kushinda taji lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa Tangu mwaka 2015 baada ya kuondoka Barcelona ambayo ilikuwa ikiporomoka kila mwaka.