Saturday, March 15

TIMU YA MAKOONGWE FC YAITANDIKA MCHINGA FC BAO 2-1.

TIMU YA MACHINGA FC
HIVI NDIO AMANI INAVYOHITAJIKA MCHANGANYIKO WA TIMU YA MAKOONGWE FC NA MACHINGA FC, kauli biu “Amani Yetu, Konsho yangu”
TIMU YA MAKOONGWE FC

NA ABDI SULEIMAN.

TIMU ya Makoongwe FC imeweza kuibuka kidedea kwa kuitandika timu ya Machinga FC bao 2-1, katika bonanza la msafara wa vijana kuhamasisha amani na utengamano wa jamii, mchezo uliofanyika katika kisiwa cha Makoonge Wilaya ya Mkoani.

Mchezo huo ulioshudiwa na mashabiki wengi wa soka katika Kisiwa cha Makoongwe, huku wenyeji wakidhamiria kuubakisha ushindi ndani ya Kisiwa chao.

Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi kubwa, kila timu ikihitaji ushindi ilichukua dakika 10 kwa Ali Khamis Mohamed kupachika bao la kwanza, kabla ya dakika 29 kuandika bao la pili.

Kipindi cha pili kilianza kwa kusisimua kwa kila timu kuonyesha ufundi wake, Machinga FC waliweza kupata bao la pekee kwa mkwaju wa Penant lililopachikwa wavuni na Ali Said Ali dakika ya 67.

Kepten wa timu ya Machinga FC Markus Sixmund Nziku, aliipongeza taasisi ya Norwegian Church Aid Tanzania kupitia mradi wa utengano wa jamii na Amani Zanzibar, kuwakutanisha vijana wa Machinga FC na Makongwe FC katika suala zima la kudumisha amani.

Alisema amani ndio kila kitu hivyo vijana wanapaswa kuwa wazalendo na walinzi wakubwa wa suala zima la Amani na kutokukubali kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.

Naye kepteni wa Makoongwe FM Ali Khamis Mohamed, alipongeza Taasisi za KKT, DMP na ZANZIC kwa ushirikiano na NCA kupitia ufadhili wa Norway kuandaa mchezo huo kwa vijana.

MWISHO