Thursday, January 16

Sanaa yarindima Wete.

WANAFUNZI wa Skuli ya msingi Kojani wakiimba wimbo katika mashindano ya elimu bila malipo, Wilaya ya Wete huko katika viwanja vya Skuli ya Sekondari M/mdogo
WANAFUNZI Skuli ya Sekondari Mchanga mdogo Wilaya ya Wete wakiimba wimbo katika mashindano ya elimu bila malipo Wilaya ya Wete huko katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Mchanga mdogo, Pemba

(PICHA NA SAID ABDULRAHMAN PEMBA)

 

NA SAID ABRAHAMAN.

MASHINDANO ya elimu bila malipo Wilaya ya Wete Kwa Kanda ya Mashariki yameendelea tena mwishoni juma lililopita kwa upande wa sanaa, kwa skuli za msingi na sekondari.

 

Michezo ambayo ilifanyika hapo ni pamoja na sanaa ya ushauri, utenzi, wimbo, ngonjera pamoja na tamthilia ambapo Skuli hizo ziliweza kutoa burudani mwanana kwa watazamaji waliofika katika viwanja hivyo.

 

Katika sanaa ya ushauri, mshindi kwa upande wa msingi iliweza kuchukuliwa na Skuli ya Minungwini ambayo ilijipatia alama 175 sawa na asilimia 87.5%, nafasi ya pili ikinyakuliwa na Mjini Kiuyu kwa kupata alama 155 sawa na asilimia 77.5% huku mshindi wa tatu ikiwa ni Skuli ya Jojo ambayo ilijipatia alama 151 sawa na asilimia 75.5%.

 

Kwa upande wa Sekondari washindi ni M/Mdogo ambayo iliahinda kwa alama 158 sawa na asilimia 79%, Minungwini ikapata alama 155 sawa na asilimia 77% huku Kangagani ikajipatia alama 149 sawa na asilimia 74%.

 

Kwa upande wa utenzi, mshindi kwa msingi ni Minungwini ambayo ilipata alama 170 sawa na asilimia 88%,Mjini Kiuyu ikajinyakulia alama 142 sawa na asilimia 71% huku Kojani ikajipatia alama 137.5 sawa na asilimia 68.75%.

 

Ama kwa Sekondari washindi ni M/mdogo ambapo walipata alama 174 sawa na asilimia  87%, Kojani alama 140 sawa na asilimia 70% huku Minungwini ikapata alama 139 sawa na asilimia 69.5%.

 

Kwa upande wa wimbo, washindi kwa msingi ni Kangagani ambao walipata alama 149 sawa na asilimia 74%, Mjini Kiuyu alama 147 sawa na asilimia 73.5% na Kojani alama 134 sawa na asilimia 67%.

 

Kwa Sekondari washindi ni Kangagani ambao walipata alama 158 sawa na asilimia 79% huku Minungwini ikapata alama 122 sawa na asilimia 61%.

 

Kwa upande wa ngonjera ambayo ilishindaniwa na Sekondari tu washindi walikuwa ni M/mdogo ambao walipata alama 148 sawa na asilimia 74% huku Minungwini ikapata alama 126 sawa na asilimia 63%,

 

wakati tamthilia ikiwa na mshindi mmoja kwa Sekondari na na msingi, Skuli ya msingi M/mdogo ambayo iliweza kupata alama 107 sawa na asilimia 53.5%.

 

MWISHO.