Monday, November 25

Jamii yatakiwa kushirikiana ili kukomesha vitendo vya udhalilishaji.

NA ABDI SULEIMAN.

 

JAMII imeshauriwa kushirikiana kwa pamoja katika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia wa wananwake na watoto, ili jamii iendelee kuishi katika hali ya amani.

 

Alisema iwapo jamii itakubali kusimama kidete na kuunda mikakati ambayo itaweza kufanikisha kutokomezwa kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia watoto wataishi kwa amani na utulivu.

 

Ushauri huo umetolewa na Afisa Utetezi na Mawasiliano kutoka taasisi ya NCA Tanzania Nizar Selemani Utango, kwenye mkutano wa msafara wa vijana wa kuhamasisha amani na mtengamano wa jamii, kupitia utekelezaji wa mradi wa mtengamano wa jamii na amani Zanzibar unaotekelezwa na taasisi za kidini, huko Tumbe Wilaya ya Micheweni.

 

Alisema suala la amani na utulivu ni jambo la uhimu sana kwa matifa yoyote duniani, wala hakuna sehemu yoyote ambayo amani hiyo inaweza kununuliwa pale inapopotea.

 

Aidha alisema vitendo vya ukatili wa kijinsia ni miongoni mwa vitendo, vinavyoweza kusababisha migogoro na kuvunja amani, pale vinapofanyika katika familia.

 

“Ndugu zanguni sisi leo tupo hapa, lengo letu ni kuhamasiasha amani kwa kuwahamasisha Vijana na kinamama, kujihusisha na kilimo kinacho stahamili mabadiliko ya tabia nchi,”alisema.

 

Kwa upande wake Muakilishi kutoka taasisi za kidini zinazoshirikiana katika kutunza amani Zanzibar, Profesa Issa Haji Zidi, alisema amani ni jambo kubwa na hatuna budi kuwa nayo katika maisha ya kila siku na sio kusubiri mapaka kunatokea tatizo.

 

Alisema siasa isiwe sababu ya kutupelekea na kuivunja amani, kwani dini zote zinahimiza suala zima la amani katika jamii, huku akiwataka viongozi wa siasa kutokuwa amstari wambele kuharibu amani.

 

Naye Shekhe Yussuf Abdalla alisema NCA imefanyaka kazi na taasisi za kidini kwa lengo la kuleta maendeleo ya uswa wa kijamii.

 

Mapema Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya, aliwataka vijana kujiepusha na vikundi vya utumiaji wa madawa ya kulevya na kwamba wazitumie fursa za kiuchumi zinazotolewa na mashirika mbali mbali.

 

Aliwataka vijana hao kuhakikisha wanashikilia fursa hiyo na kuona kuwa wanathamani kubwa kwa jamii katika kuendelea na kushirikiana katikaujenzi wa taifa.

 

Hata hivyo aliwataka vijana kuwa mstari wa mbele katika suala zima la kukemea vitendo vya udhalilishaji ambavyo waathitika wakubwa ni wanawake na watoto.