Monday, November 25

RC-Salama: Suala la usajili wa ardhi litaweza kuondoa kesi za migogoro ya ardhi.

NA SAID ABRAHMAN.

 

IMEELEZWA kuwa usajili wa ardhi ni njia moja wapo, ambayo itaweza kupnguza au kuondoa kabisa migogoro ya ardhi katika jamii.

 

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salam Mbarouk Khati, katika hutuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Wete Hamad Omar, wakati alipokua akifungua mkutano wa siku moja wa kujadili masuala ya ardhi na kufanyika katika ukumbi wa jamhuri Holi Wete.

 

Alisema kuwa kesi nyingi ambazo zipo katika Ofisi za Wilaya ni kesi za migogoro ya ardhi, ambapo zikifuatiliwa kesi hizo kwa undani utaona vielelezo vinavyoonesha umiliki wa eneo husika haupo.

 

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alifamisha kuwa, uwepo wa suala la usajili wa ardhi litaweza litaweza kupunguza au kuondoa kabisa tatizo hilo.

 

“sisi viongozi tusiwe ni wadau wakubwa tunaokaribisha, hii migogoro na badalayake tuweze kutoa kinga ya kuondosha migogoro katika jamii zetu,” alisema.

 

Hata hivyo Hamad alieleza kuwa haipendezi, kuona kiongozi anahusishwa kwa njia moja ama nyengine katika suala zima ya migogoro ya ardhi na hii ni kinyume na taratibu za kisheria.

 

“Mara nyingi ninapokuwa na Masheha wa Wilaya hii, huwa ninawasisitiza wasikubali kuwa wao ndio chanzo Cha migogoro ya ardhi na wala wasilalamikiwe wao,” alisema Hamad.

 

Aidha mkuu huyo aliwataka washiriki hao kujidhibiti na wawe na uhakika, kwa watachokifanya kiwe kisheri na wasijiingize katika migogoro isiyo ya lazima, itakayopelekea kusababisha hasara kjwa mtu mmoja mmoja.

 

Mapema Ofisa Mdhamini tume ya Mipango Khamis Issa, alieleza kuwa mpango huu ni mzuri na utaweza kusaidia kuondoa kabisa kesi za migogoro ya ardhi ambayo kwa Sasa imekuwa ni mingi mno.

 

Akitoa mada katika mkutano huo, Mrajis wa ardhi Zanzibar Dk, Abdull Nasser alisema faida kubwa inayopatyikana baada ya ardhi kusajiliwa ni kuwa dhamana ya serikali.

 

Alisema endapo ardhi itapimwa itaweza kutoa fursa kwa Serikali, kupekeka miundo mbinu yake kwa uhakika ili wananchi waweze kufaidika.

 

Aidha aliwataka wananchi ambao tayari wameshapimiwa maeneo yao, wanapaswa kwenda kuja kuchukuwa hati zao wakati zimeshakuwa tayari.

 

Katika mkutano huo jumla ya mada kuu mbili ziliwasilishwa kwa washiriki hao ikiwa ni pamoja na ‘Historia ya utambuzi na usajili wa ardhi pamoja na Faida za utambuzi na usajili na Changamoto zake.