
Rais Dk. Mwinyi aliitembelea ujenzi wa barabara unaoelekea katika maeneo huru ya vitegauchumi Micheweni na kufika eneo la Maziwangombe na kuwaeleza wananchi wa Micheweni kwamba fursa za ajira zitakapoanza wao watapewa kipambele.
Aliwataka wakuuwa Mikoa na Wilaya kwa kila Wilaya kutafuta maeneo ya uwekezaji huku akisisitiza kwamba kuna haja ya eneo hilola Micheweni kuweka viwanda vinavyohusiana na uchumi wa buluu zaidi kutokana na mazingira yake.
Rais Dk. Mwinyi alieleza haja ya kusogezwa wka huduma nyengine muhimu zikiwemo maji na umeme ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kurahisisha uwekezaji katika eneo hilo na kuwataka Wizara husika kupanga na kuweka fedha kwa ajili ya mchakato huo.
Alisema miezi minane kwa barabara ya kilomita 2.8 iliyoelezwa na wajenzi wa barabara hiyo kutoka uongozi wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ni mingi sana na kuutaka wapunguze ili shughuli ziweze kuendelea
Alisisitiza kwamba ahadi zote zilizotolewa wakati wa Kampeni zitafanyiwa kazi huku akieleza haja ya kujengwa barabara yote badala ya kujengwa eneo hiyo ya ambayo ujenzi wake unaendelea hivi sasa.
Alieleza azma ya Serikali ya kuweka viwanda katika eneo hilo kwa ajili ya kupata ajira zikiwemo zile ajira 300,000 zilizoelezwa katika Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 ili nyengine zitoke katika eneo hilo huku akiwapongeza wananchi wa Micheweni kwa kuupokea mradi huo.
Mapema Mkurugenzi waUwezeshaji na Maendeleo ya Uwekezaji ZIPA, Shariff Ali Shariff alimueleza Rais Dk. Mwinyi mipango na mikakati iliyowekwa na ZIPA juu ya eneo hilo la uwekezaji.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib kwa niaba ya wananchi wa Micheweni alitoa shukurani kwa Rais Dk. Mwinyi kwa uwamuzi wake wa kuijenga barabara hiyo na kusema kwamba wananchi wamefarajika
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar