Friday, November 15

ZAC wakutana na vijana kutoka taasisi zinazofanya kazi na Vijana Kisiwani Pemba.

NA ABDI SULEIMAN.

KAIMU Mratib wa Tume ya Ukimwi Pemba Ali Mbarouk Omar, amesema kuwa taasisi zinazofanya kazi na vijana, zinafanya kazi kubwa kupambana na tabia hatarisi zinazowalenga vijana ikiwemo mabadiliko ya tabia.

Alisema tabia hizo hatarishi zinapelekea vijana kupata maambukizi ya VVU na magonjwa ya kujamiana, sambamba na kuendelea kutoa Elimu ya afya ya Uzazi, mabadiliko ya tabia, elimu ya Ukimwi, elimu ya kujikinga na magonjwa mengine ya maambukizi ikiwemo kujamiana.

Ali Mbarouk aliyaeleza hayo wakati alipokua akizungumza na vijana kutoka taasisi mbali mbali zinazofanya kazi na Vijana Kisiwani Pemba, huko katika ukumbi wa Tume ya Ukimwi Chake Chake Pemba.

Alisema lengo la Mkutano huo ni kupokea ripoti za utekelezaji na kuwasaidia wao kuweza kusaidiana kubadilishana rasilimali na uzoefu na mambo wanayoyafanya.

“Kunataasisi nyingi zinafanya kazi na vijana, vijana ndio wahanga wakubwa wa madawa ya kulevya, ukimwi na tabia hatarishi, kuwasilisha ripoti za utekelezaji, kupanga mipango kazi ya pamoja na kueleleza vipaombele vyao watavyofanya kipindi cha miezi mitatu inayokuja”alisema.

Akizungumzia suala la Changamoto, alisema zipo kwani taasisi zinahitaji fedha kidogo, na fedha zilizokuwa zikipatikana kutoka kwa mfadhili kuhudumia shuhuli za vijana hazipatikani, huku vijana wakiendelea kufanya kazi kubwa ya kujitolea na kuweza kuwafikia vijana kuwapatia elimu rika na mambo mbali mbali.

Kuhusu mafanikio alisema ni makubwa, kwani vijana wanamwamko mkubwa wa kupima afya zao, kuzitambua tabia hatarishi zikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya na kujidunga shindano, ushoga na ubaradhuli, matendo yanayochangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya VVU na magonjwa ya kujamiana.

Akizungumzia hali ya maambukizi ya Ukimwi, alisema kisiwa cha Pemba kinaamambukizi madogo ya VVU ukilinganisha na maneo mengine, kwani tabia zinazopelekea maambukizi ya VVU kwa vijana zipo, wasichana na wanaume kuuza miili, ushoga, matumizi ya madawa ya kulevya kwa njia ya kujidunga Sindano.

Alisema pia matendo ya kujamiana kwa vijana zinapelekea kupata maambukizi ya VVU, huku mkazo mkubwa wakiuweka katika suala zima la kuwapatia elimu sahihi ya ukimwi, afysa uzazi, mabadiliko ya Tabia, kuwa vijana ili waqeze kujitambua na kuwa vijana wema ambao taifa linawategemea.

Akichangia katika mkutano huo Othaman Ali Juma kutokana mtandao wa Vijana Wete, alisema wanatoa elimu kwa vijana juu ya kujikinga na Ukimwi, huku miongozo wanayotumia sio ya kizanzibari ambayo inaweza kuleta shida wakati mwengine.

Alisema vijana wa wanaishi Pemba wanaogopa sana mimba, lakini hawaogopi kupata maambukizi ya Ukimwi, huku wakiw ana lengo la kuwafikia vijana wote wa Pemba licha ya kuanza na sheria 16 na mikakati yao ni kufikia shehia zoete za Pemba.

Naye Mratib wa Vijana Kutoka PIRO Asha Nassor Ali, alisema wameza kuwafikia vijana 150 kuwapatia stadi za maisha kwa pemba ili kuweza kujitambua.