Thursday, February 27

VIDEO: Waandishi wa habari kisiwani Pemba wapewa elimu ya umuhimu wa Chanjo watakiwa kusadia kutoa elimu kwa jamii.

KHADIJA KOMBO-PEMBA.

Jamii Kisiwani Pemba imetakiwa kufahamu kuwa upatikanaji wa chanjo ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya ili kuwanusuru wananchi wake kupata maambukizi ya maradhimbalimbaliyanayowezakuathiriafyazao.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika mafunzo ya siku mbili huko katika Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi  juu ya umuhimu wa Chanjo Mratibu Kitengo cha chanjo Pemba Bakar Hamad amesema hivi sasa Zanzibar imekabiliwa na maadhimisho ya wiki ya chanjo ambayo itaanzia tarehe 24 – 30 mwezi huu kwa kutoa chanjo mbali mbali kwa watoto na wasichana ili kuwakinga na maradhi mbali mbali yanayoweza kuyapata.

Kwa upande wake Mratibu elimu ya afya Pemba Abeid Ali Alimesema elimu juu ya umuhimu wa chanjo kwa jamii bado inahitajika ili waweze kuitikia wito pindi chanjo hizo zitakapotolewa.

Naye Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba Yakoub Mohammed Shoka amewataka waandishi kusaidia kufanya kazi hio kwani kwa nafasi yao wanaweza kuwafikia wananchi waliowengi na kupata uwelewa  kwa urahisi zaidi.

Ujumbe wa wiki ya chanjo ni jamii iliyokamilisha chanjo ni jamii yenye afya , kauli mbiu maisha marefu na yenye afya ni kwa wote.

 

ANGALIA VIDEO HII KWA KUBOFYA HAPO CHINI