Monday, November 25

ASMA MWINYI FOUNDATION yawapatia futari wananchi wa Maziwang’ombe

NA ABDI SULEIMAN.

WANANCHI wa kijiji cha Maziwag’ombe Wilaya ya Micheweni, wameishukuru taasisi ya ASMA MWINYI FOUNDATION kwa kuwapatia sadaka ya chakula kwa ajili ya futari ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Wakizungumza na waandishi wa habari, baada ya kupokea sadaka hiyo ya chakula, wameishukuru taasisi hiyo kwa kuwapatia futari hiyo, kwani kipindi cha ramadhani baadhi ya familia hali zao huwa ngumu.

Time Ali Abdalla alisema, utowaji wa futari hiyo itawasaidia katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, huku akiwaomba wahisani wengine kujitokeza kusaiida wananchi wasio na uwezo kipindi hiki cha Ramadhani.

“Hii sadaka sisi itatusaidia katika kipindi hichi, pia inamjengea njia bora ya duniani na akhera kwa aliyeitoa”, alisema.

Naye Mfaki Hamad Bakari alisema, utowaji wa futari hiyo inawaweka karibu wananchi na taasisi mbali mbali zinazojitolea kuwasaidia katika maeneo tafauti.

Hata hivyo wameiyomba taasisi hiyo, kuendelea kuwasaidia kwa kila watakacho barikiwa na Mwenyezi Mungu, kwani malipo watapata kutoka kwake.

“Kipindi hiki hali za wananchi baadhi ya ameneo yanakuw angumu, nafuu inapatikana pale taasisi zinapojitokeza na kuwasaidia wasio jiweza kuwapatia futari kama hiviii”alisema.

Kwa upande wake kiongozi kutoka taasisi ya ASMA MWINYI FOUNDATION  Mabrouk Abdul, alisema ni kawaida kwa taasisi hiyo kuwasaidia wananchi wenye mazingira magumu wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema kwa awamu hii futari walizotowa zitawafikia wananchi 175 wa Maziwangómbe na Mzambarautakao, kwa upande wa kisiwa cha Pemba, ambao watapata mchele, sukari, maharagwe na unga wa ngano.

“Sisi kila ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani, huwasaidia wananchi kwa kuwapatia futari katika maeneo tofauti ya Unguja na Pemba”, alifahamisha.

Aidha aliwataka wananchi hao kuendelea kuwa wamoja na kuzidisha msihkamano wao, kwa kusaidiana kupendana na hata kuombena dua.

 MWISHO