Monday, November 25

WAFUGAJI majongoo bahari ongezeni juhudi kufikia malengo

 

KATIBU wa Kikundi cha Mapape Cooperative Society Juma Said Ali, akimkabidhi majongoo ya bahari Waziri wa Uchumi na Uvuvi Zanzibar Suleiman Massoud Makame, wakati alipokitembelea shamba la majongoo lakikundi hicho huko katika bandari ya Mapape Chambani.(
WAZIRI wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Suleiman Massoud Makame, akiendelesha ngalawa mara baada ya kurudi kuangalia shamba la majongoo bahari yanayofugwa na Kikundi cha Mapape Cooperative Society kilichopo Mapape Chambani.(
WAZIRI wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Suleiman Massoud Makame (kushoto) akiwa na Afisa Mdhamini wa Wizara hiyo Pemba Dk.Salim Moahemd Hamaza, wakiangalia majongoo ya Bahari, yanayofugwa na Kikundi cha Mapape Cooperative Society kilichopo Mapape Chambani

NA ABDI SULEIMAN.

WAZIRI wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Suleiman Massoud Makame, amewashauri wanakikundi cha Mapepe Cooperative Society kinachojishuhulisha na ukulima wa majongoo bahari, kuhakikisha wanaongeza bidii katika ulimaji wa majongoo hayo ili kuweza kufikia malengo walojiwekea.

Alisema majongoo 60 kidogo wanapaswa kuonyesha umuhimu wa majongoo, hivyo kuongeza bidii katika kuongeza majongoo ikizingatiwa biashara hiyo imekua ni kubwa na inafaida duniani.

Kauli hiyo aliitoa katika bandari ya Mapape Chambani, wakati alipokua akizungumza na wanakikundi hicho na wananchi wa kijiji hicho, mara baada ya kurudi kuangalia majongoo bahari ya kikundi hicho.

Alisema hivi sasa soko la majongoo lipo kubwa duniani, gredi (1.A)kilomoja shilingi laki mbili, gredi B kilo moja laki 1.5 na gred C kilo moja shilingi laki moja.

“Wizara imeamua kuwapitia wadau wake wote wa uchumi wa buluu, zaidi wanaojishuhulisha na ukulima wa majongoo baharini, lengo ni kuangalia shuhuli wanazozifanya katika vikundi vyao”alisema.

Aidha alisema Wizara ipo tayari kuwasaidia wote waliojiengeji kwenye uchumi wa buluu, kuhakikisha wanawapatia mafunzo, pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kuwapatia boti kwa ajili ya doria.

Akizungumzia suala la mabwawa, alisema pia wizara ipo tayari kuwasaidia katika ujenzi wa mabwawa, sambamba na kuwapatia mbegu kutoka katika hachari za wizara ili kuweza kufuga majongoo bahari kisasa.

Waziri Suleiman aliwataka wanaushirika huo, kujipanga vizuri na kuwekeza akili zaidi katika ufugaji huo, kwani biashara hiyo inaweza kubadilisha maisha ya wanaushirika huo.

Kwa upande wake katibu wa Mapape Cooperative Society Juma Said Ali, alisema kwa sasa wanamajongoo 60 na malengo yao kufika 2023 kuwa na majongoo elfu 20000 ndani ya bwawa lao.

Alisema ili kufikia malengo hayo mikakati yao ni kununua vifaranga kutoka kwa wavuvi, wanajamii, wanawake hata kuagizia kwa baadhi ya wafugaji wenzao.

Hata hivyo alimuomba waziri huyo kuwasaidia boti ya kufanyia doria na vifaa vyake, kwani muda wa usiku vijana huvamia na kuwaibia majongoo yao.

Kikundi cha Ufugaji wa majongoo bahari kinachujulikana kwa jina la Mapape Cooperative Society, kilianzishwa mwaka 2021 kikiwa na wanachama 30 wanawake 15 na wanaume 15.

MWISHO