Monday, November 25

JAMII haijataka kubadili mtazamo wa kuhifadhi, kulinda mazingira

baadhi ya miti ya mikandaa au mikoko ikiwa imekatwa na wananchi kwa ajili ya shuhuli zao mbali mbali za kijamii, hali inayopelekea maji ya bahari kupata njia na kuvamia mashamba ya wakulima
baadhi ya matumbawe ambayo yanapatikana bahari, ila hivi sasa yamekuwa yakipotea kutokana na uharibifu unaofanywa na wavuvu wanaotumia baruti katika uvuvi wao
akinamama wakishiriki katika zoezi la upandaji wa miche ya mikandaa (mikoko) katika moja ya maeneo yaliyokuwa wazai, huko Ndagoni Wilaya ya Chake Chake ili kudhibiti maji ya bahari kupanda juu

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

WAKATI dunia ikielekea kuadhimisha siku ya mazingira duniani, ambayo hufanyika kila ifikapo Juni 5 ya kila mwaka.

Kuleleka ktika maadhimisho hayo, ujumbe wa mwaka huu ni “DUNIA NI MOJA”, ambapo kila nchi inaweza kutoa maoni yake, ili kwenda sambamba na ujumbe huo.

Ikumbukwe kuwa, maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, yaliamulia na mkutano wa kwanza wa Umoja wa Matifa.

Ambao ulihusu masuala ya mazingira na maendeleo, uliofanyika mwaka 1972, katika jiji la Stockholm nchini Swiden.

Maadhimisho hutoa nafasi kushiriki shughuli za kuhifadhi na usimamizi mazingira, matumizi endelevu ya rasilimali za mazingira, matumizi ya mbinu mbalimbali za kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko tabianchi.

Lakini hata kudhibiti kuenea kwa hali ya jangwa na ukame, upotevu wa bioanuai, uharibifu wa tabaka la ozoni na udhibiti wa shughuli, zisizoendelevu zinaweza kuchangia uchafuzi na uharibifu wa mazingira.

Katika kuelekea siku hiyo, Zanzibar ikiwa ni nchi iliyounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imelazimika kuwa na wiki ya kuelekea kilele cha siku ya mazingira.

Ambapo wiki hiyo imeanza tokea Mei 31 kwa shughuli mbali mbali za usafi, makongamano, midahalo na maonyesho ya vitu mbali mbali.

Wakati hayo yakiendelea kufanyika, baadhi ya asasi za kiraia, NGO’s ambazo zinazojishuhulisha na masuala ya mazingira nchini Tanzania, viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wameanza kuadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi.

Katika kuelekea kilele hicho, ni wazi kuwa kila mmoja kwa nafasi yake, anawajibu wa kutunza na kuhifadhi mazingira.

Kwa kuhakikisha anapanda miti au kutokuharibu vyanzo vya maji, ikiwa ni sehemu ya dhana nzima nini maana ya mazingira.

ASASI ZISIZO ZA KIRAIA ZINASEMAJE

Mkurugenzi taasisi ya ‘HUDEFO’ Tanzania Sarah Pima, anasema kila mtu ana mchango wa kufanya katika suala la utunzaji na ulinzi wa mazingira.

Anasema, kwani asasi zimekua zikiwashajihisha wananchi katika suala la uhifadhi na utuanzaji wa mazingira yao na kwa manufaa yao.

Suala la mazingira sio la mtu mmoja, wanafunzi, wananchi, viongozi wa dini, NGO’s, sekta binafsi, vijana, wanawake wote wananafasi, ya kulinda na kuhifadhi mazingira.

“Upo mkaa mbadala ambapo tunaweza kutumia, ili kulinda miti na kutumia majiko banifu, yataweza kusaidia sana kuhifadhi mazingira,”amesema.

Anasema kutokana na hali ya mazingira sasa ilivyo, ni wakati serikali, kutangaza matumizi ya mkaa mbadala na matumizi ya majiko banifu.

“Ukataji wa miti umeongezeka kwa kasi kubwa, kuliko hali ilivyokuwa mwaka jana, maji ya bahari yanaongezeka, matumizi ya plasiki nayo yamechukua kasi.

Na hivi sasa, licha ya kampeni mbali mbali kuendelea kufanyika na nguvu za serikali, bado zinahitajika,”alisema.

Mwakilishi kutoka taasisi ya ‘Elico Foundation Tanzania’ Sisty Basil, anasema katika miaka miwili iyopita, wameanza kuweka pampu za umwagiliaji zinazotumia sola na kuachana na pampu zinazotumia mafuta.

Lengo pamoja na kukua kwa teknologoia, lakini pia ni kulinda na kuhifadhi mazingira yetu.

Ni wakati sasa kwa taasisi za serikali na zisizo za kiserikali kuanza kushirikiana, katika suala la uhifadhi wa mazingira kwa kuhakikisha, wanapunza matumizi ya nishati ya mafuta.

NGO’s zinafanya ili kupunguza athari za mazingira, kwa namna kubwa serikali na zinashirikiana kutokana na kufanya kazi zaidi vijijini.

Matumizi ya nishati ya mkaa na kuni, imekua ikipoteza misitu mingi, wakati umefika kutumia mkaa unaotokana na masalia ya mazao au mimea.

Lakini pia pamoja na gesi asilia licha ya gharama zake kutokuwa ndogo.

“Niwakati sasa serikali kuangalia suala la bei ya Gesi kushuka na kufika vijijini, kwa kuweka mkono wake, ili wananchi waweze kuhimili gharama na kupunguza uharibifu wa mazingira,”amesema.

Wananchi tujitahidi kutumia rasilimali, ili vizazi vijavyo viweze kunufaika rasilimali hiyo kwa manufaa ya sasa na baadae.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET) Dk.Elen Outaru, amesema JET imekua mstari wa mbele katika kushajihisha wananchi kutunza, kuhifadhi na kulinda mazingira.

Wamekuwa wakiwatumia wanachama wakwa ambao ni waandishi wa habari, kuandaa vipindi, Makala, habari na matangaazo ya kulinda na kuhifadhi mazingira.

Jukumu la kulinda mazingira ni la wananchi wote na sio taasisi moja, ipo haja kwa serikali kushajihisha wananchi juu ya matumizi ya nishati ya Gesi nchini.

“Miti imekua ikipungua siku hadi, hewa chafu zinaongezeka, yote ni kutokana na vyombo tunavyoagiza viwango vyake vimeshapungua,’’amasema.

IDARA ZA MAZINGIRA INASEMAJE

Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Zanzibar Farhat Ali Mbarouk, amewataka wananchi kuendelea kushajihishika katika suala la uhifadhi wa mazingira.

Anaona bila ya kuwa na mazingira mazuri ya fukwe za bahari, uchumi wa buluu hauwezi kueleweka, hivyo wananchi wanapaswa kuachana na tabia ya kutupa takataka za plastiki katika fukwe.

Hali ya utupaji wa chupa za plastic katika eneo la bahari ya kivunge, hali inayohatarisha maisha ya viumbe wa baharini ikiwemo samaki.

“Hivi karibuni nilifanya ziara ya kwenda eneo la kivunge, nilisikitishwa na chupa nyingi zimetapakaa, ikizingatiwa wataalamu wamesema ifikapo 2050 kutakua na taka nyingi baharini kuliko samaki,”amesema.

MABADILIKO TABIA NCHI

Zaidi ya maeneo 148 yameathiriwa na mabadiliko hayo, ikiwemo mashamba kuingia maji chumvi, visima kuwa na maji chumvi.

Lakini hata matumbawe ya baharini kuharibika kutokana na joto kali, ambapo nchi za visiwa ndio waathirika wakubwa wa mabadiliko hayo, Zanzibar ikiwemo.

“Serikali imekua ikichukua juhudi mbali mbali kwa kujenga tuta eneo la tovuni, Msuka bandarini ili kuzuia maji kutokuingia maeneo ya kilimo, na kufanya shuhuli zao mbali mbali,’’ anasema.

TAMKO LA SERIKALI KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Tanzania Dk.Selemani Said Jafo, anasema wananchi kila mmoja anawajibu wa kutunza mazingira ya nchi yake.

Anasema ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa mahali salama pakuishi kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo, wajibu huo ufanyike pasi na kusimamiwa.

Anasema utunzaji na uhifadhi wa mazingira ni jumkumu la kila mmoja kwa nafasi yake, napaswa kutunza mazingira na kuyalinda.

“Natambua nchi inakabiliwa na changamoto mbalimbali za uharibifu wa mazingira, ikiwemo vyanzo vya maji, makazi ya wanyamapori na Bioanuai, hii inasababishwa na matumizi yasiyo endelevu yanayochochewa na utegemezi mkubwa wa jamii,”anasema.

Imebainika kwamba takriban kiasi cha hekta laki nne ( 469,420) za misitu huharibiwa kila mwaka, utupaji holela wa taka pamoja na  uwepo wa athari za mabadiliko ya tabianchi.

Hali hii inaathiri maisha ya viumbe mbalimbali ikiwemo ya mifumo ikolojia, hadi sasa imeliletea taifa hasara ya  takriban asilimia tano (5%) ya Pato la Taifa.

Kwa Zanzibar maadhimisho hayo ya siku ya mazingira, kitaifa yatafanyika kisiwani Pemba, na mgeni ramsi akitarajiwa Makamu wa Kwanza wa rais Zanzibar Othman Massoud Othman.

kaulimbiu ya kitaifa  ni ”Tanzania ni moja tu: Tutunze Mazingira”.

MWANDISHI WA MAKALA HAYA ANAPATIKANA 

Abdi Juma Suleiman

Journalist/Photographer

Zanzibarleo newspaper
Chake Chake -Pemba
+255774565947 or +255718968355
+255622161506

   MWISHO