NA ABDI SULEIMAN.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud, amesema suala la kuombea nchi dua linapaswa kuwa endelevu na la muda wote, katika miskiti na maeneo mengine, kwani inchi bado inakabiliwa na matukio mbali mbali ikiwemo ya udhalilishaji.
Alisema iwapo dua itaendelea kuombwa na waumini, basi itafika wakati majanga hayo yanaweza kuondoka kabisa ikiwemo ya udhalilishaji na watoto kuishi kwa amani.
Mkuu huyo aliyaeleza hayo wakati akitoa nasaha zake, mara baada ya kumaliza dua ya pmaoja ilioandaliwa na Ofisi ya Mufti Pemba, na kuwashirikisha viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakuu wa Wilaya nne za Pemba, Maafisa wa dhamini, viongozi wa vyama vya siasa, mashekhe na wananchi wengine, huko katika uwanja wa Gombani mjini Chake Chake.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa, aliwataka wananchi na waumini mbali mbali, kuhakikisha wanapoomba dua hiyo kuingiza masuala ya upigaji vita matumizi ya madawa ya kuleva, udhalilishaji na masuala mengine ambayo hayaendani na mila za nchi.
Akizunguzmia suala la Udhalilishaji, Mkuu huyo alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inachukua juhudi mbali mbali, ikiwemo kua na mahakama maalumu inayoshuhulikia masuala ya udhalilishaji, kwani suala hilo limekua likiumiza sana juhudi zao.
Mkuu huyo alisema bado jamii haijawa tayari katika suala hilo, kwa kuripoti katika vyombo vya sheria sambamba na kushirikiana na serikali wakati wa kutoa ushahidi pale wanapohitajika.
“Polisi wakati wenu kuchukua juhudi stahiki pale tukio linapotokezea, na tayari ameshaanza kufuatialia hata mimi mwenyewe katika mamlaka zangu hali hairidhisihi kwa kiasi kikubwa,”alisema.
Akizungumzia wananchi wanaoshiriki kuwatorosha watuhumiwa wa ubakaji, mkuu huyo amesema tayari ameshaanza kuwaweka ndani wanaohusika kuwatorosha, kufanya hivyo matukio hayo yatapungua na wahusika kufikisha katika vyombo vya sheria,
“Haiwezekani sisi tumeamua kupambana na matukio hayo, halafu wananchi wanashiriki kuwatorosha watuhumiwa,nimeshatoa maagizo kuhakikisha wanaoshiriki ndio wakwanza kuwekwa ndanihadi watakapomleta mtuhumiwa,”alisema.
Katika hatua nyengine mkuu huyo wa Mkoa, aliipongeza watendaji wa mahakama Pemba kwa kasi waliyonayo katika kesi za udhalilishaji, kwani hivi sasa zinaenda vizri ndani ya mwezi kesi tano zinashuhulikiwa, pamoja na watuhumiwa kupatia hukumu.
“Tayari tumeshatoa maagizo daktari yoyote atakayemfanyia uchunguzi mwathiriwa wa udhalilishaji, akiitwa mahakamani na kushindwa kufika, daktari huyo akamatwe na kufikishwa polisi na kuhtakiwa,”alisema.
Kwa upande wa Dawa za Kulevya, Mkuu huyo alisema mikakati mizuri ipo katika kisiwa cha Pemba na tayario wanawafuatilia waingizaji, wasambazaji na wauzaji muda si mrefu watawatia mikononi na kuwafikisha katika vyombo vyua sheria, kwani dawa hizo ni hatari kwa vijana.
Naye msaidizi katibu Ofisi ya Mufti Pemba Sheikh Said Ahmad Mohamed, alisema suala la dua lisiishie hapo bali linapaswa kuwa endelevu muda wote,huku akiwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na serikali ili kufikia malengo.
Akitoa ukumbusho katika dua hiyo Shekh Abdalla Nassot Abdalla, aaliwataka wazazi kuwa karibu na watoto wao ili waweze kuzijuwa siri zao, sambamba na kutokuwapa uhuru muda wote watoto wao.