Na Raya Ahmada.
Wafanyabisha na waendesha bodaboda wametakiwa kuzitumia fursa za kiuchumi zilizotolewa na benki ya NMB kupitia kampeni ya TELEZA KIDIJITALI ili waweze kupata mikopo ambayo haina gharama.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali kwenye uzinduzi wa kampeni ya teleza kidijitali na benki ya NMB unatowa huduma ya mshiko fasta, NMB pesa wakala, lipa namba, mkopo master bodi na mkopo master boda wakiwa na lengo la kuwakombowa wananchi kiuchumi.
Amesema mara nyingi wananchi hukumbwa na changamoto ya upatikanaji wa mikopo na kusaidiwa katika shughuli za uzalishaji, hivyo waifanyie kazi fursa hiyo.
Akizitangaza huduma za kampeni hiyo Meneja wa Biashara za NMB Kanda ya Zanzibar Naima Said Shaame amesema lengo ni kupata huduma bora na haraka kupitia simu za mkononi.
Mwenyekiti wa jumuiya ya bodaboda Mkoa wa Kusini Pemba Kassim Juma Khamis amesema hatua ya benki ya NMB kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu kwa waendesha bodaboda na bajaji imetanua wigo katika kisiwa cha Pemba.
KUANGALIA VIDEO YA HABARI HII BOFYA HAPO CHINI