Thursday, January 16

WANANCHI ndagoni watoa ya moyoni kwa idara ya katiba na msaada wa kisheria

NA ABDI SULEIMAN

WANANCHI wa Shehia ya Ndagoni Wilaya ya Chake Chake, wamesema ujio wa wanasheria kutoka Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar katika shehia yao wameupokea kwa mikono miwili, kwani wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mbali mbali.

Wananchi hao wamesema ujio wao umeweza kuwafungua macho na kujuwa matatizo yao sehemu gani waweze kuyafikisha na kupatiwa ushauri, tafauti na ilivyokuwa awali.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, kwa nyakati tafauti mara baada ya ufungaji wa kambi ya siku mbili ya wiki ya msaada wa kisheria huko ndagoni.

Omar Ali Makame Mkaazi wa shehia ya Ndagoni, alisema ujio wao uwameupokea vizuri na wamepata kufikisha kila, dukuduku lililokua likiwakabili na kupatia ushauri wa kisheria.

Alisema ujio wao isiwe mara ya kwanza kwani wananchi wa vijiji I wakabalikiwa na kero nyingi, zinazohitaji ufafanuzi wa kisheria katika utatuzi wake.

“Huku kuna baadhi ya maeneo yetu ya ardhi yamechukuliwa, sisi tulikuwa tunalima tokea Rais Jumbe wala hakuna mtu aliyetuzuwia, ila hivi sasa tumepingwa marufuku kufanya kitu chochote jambo ambalo limetukera sana,”alisema.

Akizungumzia suala la udhalilishaji, Omar alisema umefika wakati kwa sheria hiyo kufanyiwa marekebisho ili kuwatia hatiani wahusika wote wawili, kwani kumfunga mwanamme pekee ni kumuonea wakati wahusika ni wote wawili.

“Hapa kijijini kwetu tumeshamfukuza mtoto wakike kutoka Mkoani, amekuja huku mtoto miaka 22 amekuja kufata nini kama si mtu wake, halafu sheria inamtambua mwanamme tu wakati huyu msababisha haimuoni,”aliongeza.

Naye Ali Khamis Ali alisema kilio kikubwa chake ni suala zima la mirathi na ameweza kuelekezwa njia za kufuata ili kuweza kupata haki zake.

Kwa upande wake afisa Dawati la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Zuwena Hamad Ali, alisema mwitikio wa wananchi wa Ndagoni ni mkubwa, kilio kikubwa ni suala la mabadiliko ya sheria inayowatia hatiani wabakaji.

Alisema tatizo jengine ni uchukuliwaji wa ardhi yao, yakiwemo maeneo ya kilimo na kupelekea kusitisha kwa shuhuli zao za kilimo jambo ambalo linarudisha nyuma maeneo yao.

Afisa kutoka Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar Bakar Omar Ali, jumla ya wananchi 85 wamepatiwa elimu mbali mbali za kisheria katika shehia ya ndagoni, wakiwemo wanaume 43 na wanawake 42.

Alisema wananchi hao walikuw awanakabiliwa na matatizo mbali mbali, ikiwemo ardhi, utelekezwaji, mirathi, na wizi wa mifugo na mazao.

Hata hivyo aliwataka wananchi hao, kuhakikisha wananapokua na matatizo ya kisheria kuwatumia wasaidizi wa sheria waliomo katika shehia zao, ili kuwaelekeza sehemu za kwenda kufikisha vilio vyao na kupatia ufumbuzi wake.

MWISHO