Mkurugenzi wa UTPC Abuubakar Karasan akiwasilisha maelezo ya vipi Press Club zilivyokumbana na changamoto ya ukosefu wa fedha na vipi ziliweza kufanya kazi zake.
NA Bakar Mussa, Dodoma.
Ubalozi wa Sweeden umesema utaendelea kupatia ufadhili wa fedha Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kwa ajili ya kuendeleza Klabu zao kwa muda wa miaka mitatu ijayo.
Akizungumza na baadhi viongozi wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania na uongozi wa UTPCÂ kaimi Balozi wa Sweeden Mardem Sandra huko katika ukumbi wa Royal Hotel Dodoma alieleza kuwa amevutika na jinsi ya vilabu vya waandishi wa habari unavyotumia misaada yake kwa ajili ya kuendeleza tasnia ya waandishi wa habari nchini.
Alifahamisha kuwa ubalozi huo utaendelea kutowa misaada yake kwa ajili hiyo kwani inatambuwa umuhimu wa waandishi wa habari katika kukuza maendeleo.
“Nafarajika sana kuona waandishi wa habari Tanzania munatumia tasnia hii katika kuihabarisha jamii mambo mbali mbali yanayotokea Duniani”, alisema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania,Degrotius Msokolo wakati akifunguwa mkutano huo wa siku mbili aliishukuru ubalozi wa Sweeden kwa misaada yake inayoitowa kwa UTPC.
Alisema UTPC utaendelea kutowa mashirikiano na ubalozi huo katika kutumia misaada hiyo kwa ajili ya kuendeleza tasnia hiyo muhimu ya habari kwa ajili ya kuleta mageuzi makubwa ya kihabari kwa kuwajengea uwezo wanachama wake.
“Nachukuwa fursa hii kuupongeza Ubalozi wa Sweeden (SIDA) kwa kutupatia misaada kwa muda mkubwa”, alieleza.
Kwa upande wa Wenyeviti wa Press Club akiwemo Burhan Yakoub wa Tanga Press Club,Pendo Mwakiembe kutoka Mara Press Club waliipongeza SIDA kwa kuzilea Press Club kwa muda mrefu kwa kusaidia mambo mbali mbali ikiwemo vifaa kwa ajili ya kuendeleza tasnia ya habari nchini na kuwataka waendelee kufanya hivyo.
Aidha mkurugenzi wa UTPC Abuubakar Karasan aliwataka Wenyeviti wa Press Club nchini kumpatia mashirikiano mkurugenzi mpya anaekuja Kenneth Sembaya katika kuitumikia UTPC wakati yeye akiwa katika harakati za kumaliza utumishi wake hapo mwezi Disemba mwaka huu.
Hata hivyo Sembaya iliwashukuru UTPC kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo ya ukurugenzi na kuwaomba wampatie ushirikiano wao katika kuendeleza tasnia ya habari Tanzania.
MWISHO.