Thursday, January 16

BANK ya NMB yaikabidhi mashine 50 Wizara ya Utalii Zanzibar kwa ajili ya ukusanyaji wa fedha

 

MKUU wa Kitengo cha Biashara kutoka Bank ya NMB Filbert Casmir (kushoto), akimkabidhi mashine ya kupokea malipo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Dk.Amina Ameri Issa, hafla ya makabidhiyao iliyohudhuriwa na watendaji mbali mbali wa Bank hiyo na Wizara ya Utalii na kufanyika hoteli ya Serena Zanzibar.

ZANZIBAR.

JUMA ya Mashine 50 za kupokea malipo kwa Wizara ya Utalii na Mapo ya Kale Zanzibar, kwa lengo la kuongeza ukusanyaji wa mapoto kupitia sekta hiyo.

Akikabidhi mashine hizo kwa Uongozi wa Wizara ya Utalii Zanzibar, Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka NMB Filbert Casmir alisema benki hiyo inatambua mchango wa sekta ya utalii kwa uchumi wa Zanzibar.

Hala hiyo ya makabidhiano ya mashine imehudhuriwa na watendaji mbali mbali kutoka NMB na Wizara ya Utalii Zanzibar na kufanyika katika ukumbi wa hoteli ya serena jijini Zanzibar.

Mkuu huyo wa kitendo cha Biashara, alisema mfumo huo utasaidia Serikali kutambua mapato yanayokusanywa kwa mwezi katika vituo vyote vya utali nchini.

“Tumeamua kuja kukabidhi mashine hizi kwa vile tunatambua umuhimu wa sekta ya utalii katika kuinua uchumi wa Zanzibar,  sasa lazima tukusanye kwa kutumia mnjia ya mtandao,”alisema.

Hata hivyo alisema mshine hizo zinauwezo wakutumia mitandao yote ya simu, kwani ziko na ubora wa hali ya juu tafauti na mashine nyengine.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Dk.Amina Ameri Issa, aliipongeza bank ya NMB kwa ujasiri wao wakuwapatia mashine hizo za kupokelea malipo, kwani zitaweza kuwasaidia katika kuhakikisha fedha zinakusanywa kwa njia za kisasa.

Alisema kuwepo kwa mifumo ya kisasa ya ukusanyaji wa mapato  katika sekta ya utalii, kutaiadia Serikali kuimarisha uchumi wake kupitia sekta hiyo.

“Sote tunajuwa hivi sasa serikali yetu inapinga ukusanyaji wa mapoto kwa kutumia fedha mkononi, lazima mapato yote yapitie nijia za kieletroniki, mashine hizi zitatusaidia kwa kiasi kikubwa,”alisema.

Aidha alifahamisha kwamba, mashine hizo zitasaidia kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato, na hivyo kuondosha changamoto zilizokuwa zikijitokeza awali.

Hata hivyo Naibu katibu Mkuu, aliishukuru benki ya NMB kwa kuwa mdau mkubwa wa kushirikiana na kuisaidia serikali, katika sekta mbali mbali za kimaendeleo ikiwemo sekta ya utalii.

Jumla ya mashine 50 zimekabidhiwa kwa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, ambapo mteja anaweza kulipia kupitia mitandao yote ya simu na kwa njia ya kadi.

MWISHO