NA ABDI SULEIMAN.
MKURUGENZI wa Utafiti Tume ya Taifa ya Mipango na Mtumizi ya Ardhi Tanzania Dr.Joseph Paul, amesema bado jamii haijaona umuhimu wa mpango wa matumizi ya ardhi wakati wao ndio wanaoathirika.
Alisema kuna baadhi ya vijiji bado wananchi wanaficha madhara wanayoyapata yanayotokana na Tembo, wakihofia maeneo yao kutengwa na kuwa mapitio ya wanyamapori(Shoroba).
Mkurugenzi huyo aliyaeleza hayo Mkoani Dodoma, wakati wa ziara ya waandishi wa habari wa JET juu ya kufanya mahojiano na wakuu wa taasisi mbali mbali zinazohusika na Uhifadhi, iliyoandaliwa na JET chini ya mradi wa Tuhifadhi Maliasili Tanzania kutoka shirika la misaada la watu wa Marekani (USAID).
Alisema Tembo walivyokua hatari katika maisha ya binaadamu, baadhi ya vijiji vinashindwa kutoa taarifa ya madhara ya Tembo, sababu wanahofia eneo lao kuwa koridoo wakati eneo linalobakia linakua salama.
Aidha alisema tume inaendelea kuijengea uwelewa jamii kuona kuna umuhimu wa kua na mipango ya matumizi ya ardhi, kwani rasilimalizi zilizopo zinapaswa kuhakikishwa matumizi yake yanakua endelevu, lazima kuwe na mipango ya matumizi ya ardhi, rasilimali za misitu, mifugo, maliasili.
Akizungumzia majukumu ya Tume ni kusaidia wezeshaji wa uwandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi, ili kulinda rasilimali zilizopo na kuhakikisha kwamba matumizi mengine ya ardhi yanakua endelevu na matumizi yaliyopo kwenye uhifadhi, kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijanvyo.
Kwa upande wa lengo alisema ni kuhakikisha wanalinda rasilimali za maliasili zilizopo na kuhakikisha maisha na maendeleo ya wananchi wa kawaida zinaendelea kila siku.
kwa upande wa suala la uhifadhi, Mkurugenzi huyo alisema katika siku za hivi karibuni maeneo yaliyohifadhiwa wanyama wameongezeka, matumizi ya shuhuli za kibinaadamu yanahusiana kwa ukaribu na matumizi yake yasiathiriwe na maeneo ya hifadhi.
“Vijiji vinavyozunguka maeneo ya hifadhi vinaandaliwa mipango ya matumuzi ya ardhi, huwezi kuweka nyumba kwenye maeneo ya uhifadhi, sawa sawa kupanda mbogamboga kwenye mapito ya Tembo,”alisema.
Alisema kuna kampeni kubwa ya kuvutia utalii, wanaandaa mipango ya matumuzi ya ardhi ambayo italinda rasilimali za maliaasili na wanyamapori waliopo, pamoja na maumbile na kuandaa mipango ambayo yataruhusu kukuza utalii, kwani wamekuwa wakitenga maeneo ya uwekezaji na kuboresha maisha ya wananchi wa maeneo husika ikiwemo ufugaji wa nyuki.
Katika hatua nyengine Mkurugenzi Paul, alisema JET imeona mumeona umuhimu wa mipango ya ardhi kwa ajili ya kulindsa mazingira, hivyo aliwataka kusaidia kuelimisha uma juu ya umuhimu huo, kwani utasaidia kupunguza migogoro ya matumizi ya ardhi kwa kiango kikubwa katika ameneo ambayo yameshaandaliwa.
Naye Afisa Mipango Mjini kutoka Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania Mapambano Madebo Bizuru, alisema changamoto kubwa inayokabili ni ugawanyikaji wa vijiji mara kwa mara, migogoro ya ardhi kwa wanavijiji, licha ya Tume kuendelea kutoa elimu kwa wanavijiji juu ya sheria ya mazingira.
Alisema changamoto nyengine miradi mingi inaibuliwa juu baada ya kuibuliwa chini kwa wanavijiji, wakati kisheria miradi yote inapaswa kuibuliwa chini na sio juu kama inavyofanyika.
Hata hivyo alisema bado serikali na wadau mbali mbali, wanatakiwa keekeza katika elimu kutasaidia suala zima la uhifadhi na ulizi wa matumizi ya ardhi na kua endelevu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa JET Tanzania John Chikomo, alisema lengo la ziara hiyo kwa waandishi ni kufanya mahojiano na viongozi wa taasisi zinazohusika katika masuala ya uhifadhi, ili kuhakikisha matumizi ya ardhi yanakua endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo, pamoja na uhifadhi mzuri wa mazingira nchini.
MWISHO