Friday, January 10

Maadhimisho ya miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar – Huduma bora kwa jamii

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla alisema muendelezo wa Miradi mbali mbali inayoanzishwa na Taasisi za Umma na hata ile ya Wananchi inazidi kuijengea uwezo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutoa huduma bora za Kijamii kwa Wananchi wote bila ya Ubaguzi.

Akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Wananchi kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hapo Viwanja vya Mnazi Mmoja Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman alisema Wananchi  ndio wadau Wakubwa  wa kuvuna Matunda ya Mapinduzi kupitia Miradi hiyo.

Mheshimiwa Hemed ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa alisema Sherehe za Mapinduzi za Mwaka 2021 ilijumuisha Matukio 18 yaliyotanguliwa na usafi wa Mazingira uliopokelewa vyema na Wananchi katika maeneo yao chini ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote.

Alisema Miradi Tisa ya Maendeleo ndani ya shamra shamra za maadhimisho hayo ilizinduliwa na Miradi Mitatu kuwekewa Mawe ya msingi inayokisiwa kuwa na gharama ya Jumla ya Shilingi Bilioni Arubaini na Sita, Mia Moja na Sabini ya Tisa Milioni, Laki Tisa, Ishirini Elfu na Ishirini {46,179,920,020/-}.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Wananchi kwamba Miradi hiyo Mitatu iliyowekewa Mawe ya Msingi inamalizika kwa muda uliopangwa na kuonya mapema kwamba Serikali Kuu haitokuwa na muhali kwa kuwachukulia hatua za Kisheria  mara moja wale wakaozorotesha kukamilika kwa Miradi hiyo hasa suala zima la tabia ya kuchomoa fedha ndani ya Miradi hiyo.

Mheshimiwa Hemed Suleiman alitoa shukrani maalum  za dhati kwa Wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa kushiriki kwa wingi na kikamilifu kwenye matukio mbali mbali ya Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 kutimia Miaka 57.

Alifahamisha kwamba kujitokeza kwa wingi kwa Wananchi hao kunaonyesha wazi wapo tayari na timamu kuendelea kuyalinda Mapinduzi Mapinduzi hayo yaliyolenga kumkomboa  Mwananchi wa Zanzibar kutokana na unyonge na madhila ya kutawaliwa.

“ Wakati tunaadhimisha siku hii ya leo kunawakumbuka pia Wazee wetu waliopoteza maisha yao kutukomboa na leo hii tupo huru tutaendelea kuwa hura kwa sababu Mapinduzi Daima na Tutayalinda. Potelea Mbali”. Alisema Mh Hemed Suleiman

.

 

 

Halkadhalika Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa aliwapongeza Wajumbe wa Kamati hiyo kwa maandalizi na usimamizi mzuri wa Maadhimisho ya Miaka 57 ya Mapinduzi,

Pongezi kama hizo pia Mheshimiwa Hemed Suleiman Alizielekeza  sambamba na Kundi la Wanahabari kwa kazi zao nzuri zilizofanyuikisha kwa kutoa Habari kwa Wananchi juu ya matukio yote ya Sherehe hizo.

Mkesha wa kuamkia Tarehe 12 Januari 2021 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman alikuwa mgeni rasmi katika Sherehe za Fash Fash zilizofanyika katika Uwanja wa Maisara Suleiman.

Maelfu ya Wananchi kutoka pembe zote za Wilaya za Unguja sambamba na Mikoa Miwili wa Pemba walioanza kuwasili tokea jioni wameshuhudia fash fash hizo zilizokuwa burdan tosha ndani ya Mkesha huo wa Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 kutimia Miaka 57.

Sherehe hizo za aina yake zinazozidi kupamba moto kila Mwaka  zilipambwa na Burdani ya Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar sambamba na muziki maarufu unaopendwa na Vijana ule wa Kikazi Kipya.

 


Warning: file_get_contents(): http:// wrapper is disabled in the server configuration by allow_url_fopen=0 in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48

Warning: file_get_contents(http://api.xtrsyz.org/xt-visitor-counter/default.php?domain=www.pembapress.club&time=1736493499): Failed to open stream: no suitable wrapper could be found in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48