Monday, November 25

Kombe la Dunia 2022:Kikosi cha Argentina chalazimika kutumia helikopta baada ya mashabiki milioni nne kufurika barabarani kwa sherehe

ashindi wa Kombe la Dunia wa Argentina walilazimika kuachana na gwaride la mabasi ya wazi huko Buenos Aires na badala yake wakapanda helikopta juu ya mamilioni ya mashabiki waliokuwa na furaha barabarani.

Kikosi hicho kilionyesha kombe hilo mwanzoni mwa safari iliyopangwa ya saa nane.

Lakini sherehe kwenye barabara zilizojaa zilizidi kuwa hatari, na kulazimisha kubadilishwa kwa mpango wa kutumia mabasi.

“Haikuwezekana kuendelea uwanjani kutokana na idadi kubwa ya mashabiki wenye furaha,” aliandika msemaji wa rais Gabriela Cerruti kupitia Twitter.

th

Video za mitandao ya kijamii zilionekana kuonyesha mashabiki wakiruka juu ya basi lililokuwa limebeba wachezaji wakati mmoja lilipopita chini ya daraja, huku shabiki mmoja akianguka.

Serikali ya Argentina ilitangaza Jumanne kuwa sikukuu ya kitaifa katika nchi hiyo ya Amerika Kusini baada ya Lionel Messi na wachezaji wenzake kuifunga Ufaransa katika fainali siku ya Jumapili.

Takriban watu milioni nne walipanga foleni katika mitaa ya Buenos Aires, kulingana na makadirio ya ndani.

“Leo Argentina ilipata mojawapo ya karamu ya ajabu katika historia yake. Kulikuwa na furaha na shukrani tu’ Cerruti aliongeza.

th