Friday, November 15

HABARI KATIKA PICHA:WANAFUNZU SKULI YA PUJINI MSINGI WASOMA KATIKA MAZINGIRA HAYA

IPO haja kwa Wizara ya Elimu na Serikali ya Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba, kuwafikiria kwa kina wanafunzi wa skuli ya Msingi Pujini, juu ya mazingira magumu ya kukalia darasani mwao, ili waweze kupata elimu wakiwa katika mazingira mazuri na bora ya kusomea.

skuli ya msingi Pujini ni miongoni mwa skuli kongwe ndani ya wilaya hiyo, kwa sasa inahitaji mabadiliko ya hali ya juu, mabadiliko hayo yatawasaidia hata wazazi kuwapunguzia mzigo wa kutafuta sare tatu au nne kwa mwaka kwa ajili ya mtoto wake kutokana na mazingira mabaya ya sakafu ya skuli hiyooo

WANAFUNZI Skuli ya msingi Pujini wakiwa katika mazingira magumu ya kukalia, awali viongozi wa wizara ya Elimu na skuli husika ilikataa uwepo wa suala hilo, huku kamera ya Mtandao wa Habari Potali ikishuhudia wanafunzi wakisoma darasa likiwa katika hali mbaya ya sakafu.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
SURUALI za wanafunzi zikiwa katika hali ya kuchanika kutokana na mazingira ya mabovu ya kukalia katika darasa hilo