Monday, November 25

ZEMA ZATEKETEZA TANI TATU NA KILO 450 ZA VIFUKO VYA PLASTIKI.

NA ABDI SULEIMAN.

MAMLAKA ya Usimamizi wa Mazingira Pemba (ZEMA), imefanikiwa kuteketeza kwa moto tani tatu (3) na kilo 450 za vifuko vya plastiki vikiwa na thamani zaidi ya                             shilingi Milioni 40.5.

Zoezi hilo la utekeletezaji wa vifuko vya Plastiki, limefanyikwa huko Vitongoji kwareni liwa limesimamiwa na viongozi mbali mbali wakiwemo mahakimu, ZAECA na taasisi nyengine.

Akizungumza na waandishi wa habari mara, baada ya kumalizika kwa zoezi la uchomaji wa vifuko hivyo, Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Kwanza Rais Ahmed Abubakar, alisema fedha nyingi imepotea katika vifuko hivyo, jambo ambalo linalopelekea umaskini kwa wahusika.

Aliwasihi wananchi kufanya biashara za halali ambazo serikali na wananchi inazikubali, ambazo ziko salama na zinaweza kusaidia vijana wengine kupata ajira.

“Ni fedha nyingi sana zimepotea kwa mfanya biashara, vizuri wananchi fedha kama hizo wangezielekeza sehemu nyengine, ambyo iko salama na halali kuekeza,”alisema.

Aliwataka wananchi kuendelea kutunza mazingira, ambayo yataendelea kuwafanya wananchi kubaki salama, kwani mifuko hiyo hata wanyama pia vinawaathiri baada ya kula.

Akizungumzia ukamatiji wake ni jumla ya operesheni za kawaida zinazofanywa na ZEMA, kupitia sheria NO:3/2013 kupitia kanuni yake ya 2018, ndizo zinaipa ZEMA mamlaka ya marufuku ya mifuko yote ya plastiki.

Alisema serikali imeweka kanuni na sheria hiyo ili kusimamia na wananchi wasitumie wala kusambaza mifuko hiyo, kwani ni mifuko haramu kwa matumizi ya binaadamu na inasababisha uharibifu wa mazingira.

“Licha ya kuharibu mazingira pia huharibu maeneo hatarishi yale ambayo wananchi wanaishai, vifuko pia ni hatari kwenye kilimo vinapoingia chini ya ardhi haviozi bali vinabaki na mifugo pia hatari,”alisema.

Aliwataka wananchi kufahamuwa kuwa mazingira ni wananchi wote na sio serikali pekee, kushirikiana kuhakikisha mazingira yanatunzwa, pamoja na kila mmoja kutimiza wajibu wake katika kulinda matumizi ya mifuko.

Naye Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa Mazingira (ZEMA) Pemba Abuu Jafar Ali, alisema tani 3 na kilo 260 za mifuko hiyo imekamatwa Oktoba 6 mwaka huu, katika maeneo kiuyu na zilizobakia zimekamatwa maeneo mbali mbali ya wafanyabiashara wadogo wadogo.

Alisema baada ya kukamatwa na kupelekwa mahakamani na mahkama, ikaamua ni kosa na kulipa faini na kutakiwa kuangamizwa kwa mujibu wa sheria ya ZEMA ili zisiendelee kutumika maeneo mengine.

MWISHO


Warning: file_get_contents(): http:// wrapper is disabled in the server configuration by allow_url_fopen=0 in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48

Warning: file_get_contents(http://api.xtrsyz.org/xt-visitor-counter/default.php?domain=www.pembapress.club&time=1732516458): Failed to open stream: no suitable wrapper could be found in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48