Monday, November 25

Yanga SC Yaendeleza Ubabe Ligi Kuu ya NBC Yatembeza Kichapo kwa Azam 3-2 Kwa Mkapa Jijini Dar es Salaam

Mshambuliaji wa Timu ya Yanga Sc Fiston Mayele  akishangilia bao lake dhidi ya Azam wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.Timu ya Yanga imeibuka kidedea kwa bao 3-2.

 

 

Mshambuliaji wa Timu ya Yanga Fiston Mayele akimpita beki wa Timu ya Azam katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam Timu ya Yanga imeshinda mchezo huo kwa bao 3-2.
Wachezaji wa Timu ya Yanga na Azam wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.Timu ya Yanga imeshinda mchezo huo kwa bao 3-2.

 

Ni mtanange wa kuktata na shoka ukiwakutanisha wababe wa soka Matajiri wa Jiji la Dar es Salaam kutoka Chamazi timu ya AZAM FC na Young Africans ya Jangwani Kariakoo ya Dar es Salaam.

Mchezo huo wa Ligi kuu soka ya NBC Tanzania bara umepigwa katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam ambapo timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 bao la kwanza likifungwa katika dakika ya 27 na mshambuliaji wake Hamisi Suleiman Sopu akiunganisha krosi safi ya Price Dube.

Iliwachukuwa dakika 4 tu baadaye Yanga kusawazisha bao hilo likipachikwa kambani na Mshambuliaji wa kimataifa raia wa Congo Fiston Mayele katika dakika ya 30 ya mchezo huo, na dakika 2 tu baadaye Stephae Azizi ki alipachika bao la pili dakika ya 32 kwa shuti kali llilomshinda mlinda mlango wa AZAM FC Ahmes Ahmada goli lililodumu katika kipindi chote cha kwanza cha mchezo huo.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa kila timu kulisakama lango la mwenzake ambapo timu ya AZAM kusawazisha kwa kupachika bao la pili lililowekwa kambani na Hamisi Suleiman Sopu  katika dakika ya 46 ya kipindi cha pili na kumfanya mshambuliaji huyo kutupia mabao mawili peke yake katika mchezo huo.

Timu ya Yanga ilipachika msumari wa tatu mnamo dakika ya 77 ya kipindi cha pili likifungwa na Farid Mussa Mariki akiunganisha mpira uliotemwa na Mlinda mlango wa AZAM FC Ali Ahmada kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Stephane Azizi Ki.

 

CHANZO CHA HABARI ZANZINEWS