Wednesday, January 15

RAIS DK. MWINYI AHUDHURIA TAARAB MAALUM YA MIAKA 59 YA MAPINDUZI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar.Mhe Tabia Maulid Mwita ,Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ,Sera,Uratibu na Baraza la Wawakilishi.Mhe.,Hamza Hassan Juma, alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B”Unguja kuhudhuria hafla ya Taarab rasmin ya Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar jana usiku 12-1-2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiwa katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja wakati wa hafla ya Taarab Maalumu ya Maadhimisho ya sherehe za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakiwa katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, wakati Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar kikitowa burudani katika hafla hiyo Msanii Hafidh Abdulsalam akiimba wimbo wa “Walisema Hatuwezi” ikiwa ni Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar iliyofanyika jana usiku 12-1-2023 katika ukumbvi wa hoteli hiyo.
MSANII wa Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar Hafidh Abdulsalam akitowa burudani wakati akiimba wimbo wa “Walisema Hatuwezi” wakati wa Taarab Maalum ya kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliyofanyika jana usiku 12-1-2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B”Unguja.
MSANII wa Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar.Prof Mohammed IIiyas akitowa burudani wakati akiimba wimbo wa “Hakika Ninakupenda” wakati wa Taarab Maalum ya kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliyofanyika jana usiku 12-1-2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B”Unguja.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimtunza Msanii B.Sabah Salum Muchacho wakati akitowa buduradi ya wimbo wa “Mnaminami Viumbe” wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliyofanyika jana usiku 12-1-2023,katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.(Picha na Ikulu)

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi jana usiku alijumuika na wananchi na viongozi mbalimbali wa chama na serikali kwenye taarabu rasmi ya maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo.

Taarabu hiyo ilitumbuizwa na vikundi viwili tofauti kikiwemo kikundi cha sanaa cha taifa pamoja na kikundi cha “Island Morden taarabu, maarufu kama Wajelajela” ilikua maalumu kwa kuyaenzi Mapinduzi ya mwaka 1964 pamoja na kumpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kazi kubwa aliyoifanya ndani kipindi cha miaka miwili ya uongozi kwa kuiletea Zanzibar maendeleo makubwa.

Katika hafla hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Golden Tulip, Uwanja wa ndege, Zanzibar ulipambwa kwa vifijo na hoi hoi kutoka kwa wasanii wa vikundi hivyo, aliomudu vyema kukonga nyoyo za wananchi waliohudhuria kutokana na umahiri wao wa kucharaza ala pamoja kughani nyimbo mbali mbali, zilizotoa hamasa na kupamba usiku wa Mapinduzi mbele ya Rais Dk.  Mwinyi

Wasanii nguli kutoka “Wajelajela” walifanikiwa kuitawala vyema hadhira iliyojumuika nao kwa kulidhibiti vizuri jukwaa kiasi cha kuwafanya watazamaji na wasikilizaji wao kushindwa kujizuia na kuibua vifijo na nderemo.

Miongoni mwa nyimbo zilizovuta hisia na kushangiliwa muda wote ni ile ya “Walisema hatuwezi nawaje kututizama” ulioimbwa na Ustadh Hafidh Abdulsalam, wimbo wa “Kweli nnaye” ulioghaniwa na Ustadh Iddi bin Suweid, wimbo wa  “Kimeniasiri nini” ulioimbwa na msanii mahiri (Al – anisa, Husna kitoto)  na wimbo wa “Mbona watakereka sana” ulioimbwa na (Al – anisa, Sabah Salum)

Nyimbo nyengine zilizoimbwa usiku huo ni pamoja na wimbo wa “Mapinduzi” ambao uliimbwa na wasanii wote walioburidisha hafla hiyo, wimbo wa “Mimi nae damdam” ulioghaniwa na Al-anisa, Rukia Ramadhan, “Ukewenza” uliimbwa na Al-anisa Amina Hamad na Ustadh Maliki Hamad, wimbo wa “Kama yalivyonipata” uliimbwa na (Al – Anisa, Sabina Hassan), “Hakika Nnakupenda” uliibwa na Profesa, mkongwe wa taarabu nnchini, Ustaadh Moh’d Iliyas, wimbo wa “Mkodombwe” ulitumuizwa na Al – anisa, Safia Yahya.

Naye, Ustadh Hassan Vocha akakonga nyoyo za washabiki wake kwa nyimbo za “Kupendwa na Rejea tena chuoni”, nyimbo za “Mnaminami Viumbe” na “Mbona Mtakereka sana” ambazo zilihaniwa na (Al-anisa, Sabah Salum).

Mapema, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, na Michezo, Fatma Hamad Rajab alizungumza kwenye hafla hiyo na kueleza kwamba taarabu hiyo ya kihistoria ilikua maalum kwaajili ya kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya kazi kubwa iliyofanywa na viongozi wa nchi ya ufunguzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Taarab hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Kitaifa, akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, pamoja na viongozi wengine wa chama na Serikali.

IDARA YAMAWASILIANO,

IKULU