Friday, October 18

Milele yakabidhi vifaa kwa Hospitali ya Chake Chake.

MRATIB wa Milele Zanzibar Faoundation Pemba Abdalla Said Abdalla, (kulia) akimkabidhi mashine ya kufulia nguo yenye tahamani ya Milioni 2,000,000/= Dktari Dhamana wa Hospitali ya Chake Chake Ali Omar Khalifa, hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Milele Mfikiwa Wilaya ya Chake Chake .(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

TAASISI ya Milele Zanzibar Foundation Pemba, imekabidhi mashine ya kuchemshia vifaa vya upasuwaji na nguo(auto clave), pamoja na mashine ya kufulia nguo vyote vikiwa na tahamani ya shilingi Milioni 14 kwa uongozi wa Hospitali ya Chake Chake.

Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa ni mashine ya auto clave yenye thamani ya shilingi Milioni 12 na mashine ya kufulia nguo yenye thamani Milioni mbili.

Akuzungumza katika hafla ya kukabidhi mashine hizo, kwa uongozi wa hospitali ya Chake Chake, mratib wa Taasisi ya Milele Ofisi ya Pemba Abdalla Said Abdalla, alisema taasisi hiyo imo katika harakati za kusaidia jamii katika kuwakomboa na umasikini.

DAKTARI Dhamana wa Hospitali ya Chake Chake Ali Omar Khalifa, akitia saini mkataba wa kupokea msaada wa vifaa mbali mbali kutoka Taasisi ya Milele Zanzibar Faoundatio, hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi za Milele Mfikiwa Wilaya ya Chake Chake Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

Alisema Milele imekuwa imejikita katika kusaidia sehemu tafauti ikiwemo elimu, Afya, Uchumi, ili kuwahikisha wananchi wananufaika na uondokana na matatizo yanayowakabili.

“tulipata barua yenu kwamba mumeharibikiwa na kifaa cha kuchemshia vifaa vya upasuaj na nguo zake, pamoja na mashine kuoshea nguo, tulikaa na viongozi waliopo Unguja na nje ya nchi tumeamua kuwasaidia baada ya majibu kurudi”alisema.

Abdalla alifahamisha kwamb kipindi hiki hawakua na bajeti ya vitu hivyo, kutokana na ugonjwa wa Corona ulivyoathiri na pesa nyingi kuingizwa huko, lakini kutokana na umuhimu wa hospitali hiyo imelazimu kusaidia mashine hizo.

MRATIB wa Milele Zanzibar Faoundation Pemba Abdalla Said Abdalla, (kulia) akimkabidhi mashine ya kuchemshia vifaa vya upasuaji pamoja na nguo za operetion yenye thamani ya shilingi Milioni 12,000,000/=, Dktari Dhamana wa Hospitali hiyo Ali Omar Khalifa, hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Milele Mfikiwa Wilaya ya Chake Chake .(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

Aliongeza kuwa Hospitali ya Chake Chake  ni Hospitali ya Rufaa kwa sasa, inatoa huduma mbali mbali tukaona wagonjwa wapate usalama, pia na madaktari wafanye kazi zao kwa usala, hii mashine ya kufulia nguo na kuchemshia vifaa vya upasuaji tumeona tuwapatie, huku akiwataka viongozi hao kuvitunza, kutumika kama vilivyokusudiwa kwa maslahi ya nchi.

Kwa upande wake daktari dhamana wa Hospitali ya Chake Chake Ali Omar Khalifa, aliishukuru Milele Zanzibar Foundation kwa msaada huo, kwani umefika kwa wakati muwafaka, kwa kuwajali wafanyakazi wa hospitali ya Chake Chake.

“Kwa muda mrefu tumekuwa na upungufu wa vifaa, (auto clave) na mashine ya kufulia, kwa kipindi kifupi wamefikiria maombi yetu, kipindi hiki hali ya uchumi ni ngumu kweli pia”alisema.

Hata hivyo alizitaka taasisi nyengine kujitokeza kusaidia, kwani mambo haya ni yetu sote kwa ajili ya kuimarisha afya za watu, serikali pekee haiwezi kukamilisha mambo yote pasinakuungwa mkono na taasisi binafsi.

WATENDAJI kutoka Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation Pemba, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Hospitali ya Chake Chake, mara baada ya kukabidhiwa vifaa mbali mbali vya Hospitali ya Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)