Monday, November 25

Wananchi kata ya Mkula na Mangula wataka mradi wa ushoroba umalizike waendelee na shuhuli zao za kilimo

NA ABDI SULEIMAN.

WANANCHI wa kata ya Mkula na Mangula, Wilaya ya Kilombero Halmashauri ya Mji wa Ifakara Mkoani Morogoro, wamezitaka taasisi husika kuharakishwa kwa mradi wa ushoroba uweze kumalizika kwa wakati, ili Tembo wasiendelee kuharibu mazao ambayo ndio tegemeo kwao na familia zao.

Wamesema kukamilika kwa mradi huo wa Shoroba, utakaoweza kuruhusu Tembo wanapotoka hifadhini kupita katika njia zao na kwenda hifadhi nyengine bila ya kuharibu mazao ya wananchi.

Wananchi wa kata hizo wameyaeleza hayo, wakati walipokua wakizungumza na wanadishi wa habari wa uhiofadhi wa wanyamapori na utalii kutoka vyombo mbali mbali vya habari, juu ya umuhimuwa uwepo wa shoroba iliyopita katika kata hizo, ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa USADI Tuhifadhi Maliasi unaratibiwa na JET.

Mrashi Jumbe Dongwa kutoka kijiji cha Sanjo kata ya Mkula, ambaye ni Mkulima wa Miwa na Mpunga, alisema wamelazimika kukubali ujenzi wa mradi wa ushoroba uweze kupita katika mashamba yao, ili waweze kupunguza kero ya mnyama Tembo kuharibu mazao yao.

“Tembo wamekuwa wasumbufu kwa kiasi kikubwa kwa sisi wakulima, anapotoka katika hifadhi ya Taifa ya Nyerere kwenda Udzungwa, huharibu mazao na kutishia maisha ya wananchi zaidi muda wa usiku wanapotoka”alisema.

Alifahamisha kwamba baada ya tathmini kupigwa mara ya kwanza alilipwa Milioni 11.5 shemba halikua na mazao ekari mbili (2) na mara ya pili alilipwa Milioni 12.6 ikiwa ni robo tatu shamba likiwa na miwa.

Hata hivyo baada ya wananchi kuona athari za tembo kwenye mashamba yao, wamelazimika kukubali kupisha mradi huo katika maeneo yao ili kupunguza athari zinazojitokeza.

Kwa upande wake Mohamed Ali mkaazi wa kikiji cha Kanyanja kitongoji cha mikoroshini, alisema mradi wa shoroba umepokelewa kwa 75%, huku jitihada za serikali ni kuona wananchi wanaondokana na adha ya mnyama tembo kuharibu mashamba yao.

akionyesha waandishi wa habari tembo wanakotok katika hifadhi ya taifa ya Nyerere na kupita katika mashamba ya watu na kwenda hifadhi ya Taifa ya Udzungwa

“Kinachofanywa wengi tunaelewa ushoroba wanavyokuja, inawezekana adha ya tembo ikakimbia tunaona picha watu wanaishi na mnyama tembo anapita katika njia zake bila ya kuleta madhara,”alisema.

Naye Mtendaji wa kijiji cha Sole Wendo Isdory, alisema wanawaamini mradi wa ushoroba baada ya kukamilika utapunguza changamoto nyingi za tembo, kutoka hifadhi moja kwenda nyengine na kupita katika makaazi ya watu pamoja na kuharibu mazao.

“Mwaka jana tembo walitoka hifadhini na kwenda kula tikitiki karibu ekari mbili, wanashababisha hasara kwa mkulima hata kushuka kwa uchumi wa mtu mmpoja mmoja ambao ndio tegemeo kwao,”alisema.

Mratibu wa mradi wa kuboresha mahusiano kati ya tembo na binaadamu kutoka shirika la STEP, Kim Lim alisema mpaka sasa wanavijana sita wanaofuatilia taarifa za tembo kutoka vijiji tafauti.

Mratibu wa mradi wa kuboresha mahusiano kati ya tembo na binaadamu kutoka shirika la STEP, Kim Lim, akizungumza na waandishi wa habari kutoka JET

Alisema vijana hao wameweza kufuatilia ipasavyo taarifa hizo za tembo na kutoa taarifa ambao kijiji cha kanyenja 2019 matukio 167 na 2022 matukio 300.

Kwa upande wake Meneja wa mradi wa urejeshaji wa shoroba kutoka taasisi ya STEP Joseph Mwalugelo, alisema lengo ni kuzuwia migogoro baina ya binaadamu na tembo, na kuwafanya tembo sasa kupita katika njia yake maalumu (shoroba).

Alisema hifadhi zipo muda mrefu na jamii lazime zinufaike na hifadhi hizo, baada ya kuwepo kwa njia maalumu ya kupitia wanyama tembo wanapotoka hifadhi moja kwenda nyengine.

Abdi Juma Suleiman

Journalist/Photographer

Zanzibarleo newspaper
Chake Chake -Pemba
+255774565947 or +255718968355

MWISHO