NA ABDI SULEIMAN.
WANANCHI waliolipwa fidia baada ya kutoa maeneo yao na kupisha mradi wa Shoroba, wamesema fedha walizopata wameweza kunua mashamba mengine kwa ajili ya kilimo pamoja na kuongeza biashara ndani ya maduka yao.
Walisema fedha hizo wameweza kuzitumia kwa kuekeza katika miradi mengine ambayo itaweza kuwasaidia kwa shuhuli zao mbali mbali, kwani kilimo kwao ni kitu muhimu.
Wananchi wa kata hizo wameyaeleza hayo, wakati walipokua wakizungumza na wanadishi wa habari wa uhiofadhi wa wanyamapori na utalii kutoka vyombo mbali mbali vya habari, juu ya umuhimuwa uwepo wa shoroba iliyopita katika kata hizo, ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa USADI Tuhifadhi Maliasi unaratibiwa na JET.
Mohamed Ali Libongoi mkaazi wa kikiji cha Kanyanja kitongoji cha mikoroshini, alisema baada ya kupata fedha aliamua kuziingiza katika biashara ya duka kwa kuoneza bidhaa dukuni.
Alisema fedha nyengine aliamua kuingia katika vikoba kwa ajili ya kuweka, ili kuweza kuzinusuru au kutokuzitumia kiholela hole baadae ikawa tabu kwakwe.
“Mimi nashukuru fedha iliyopwa baada ya kutoa eneo la ardhi na mukiwa na vipando, nimelazimika kuziingiza dukani hapa kwa kukuza mtaji wangu,”alisema.
Naye Isaya Fabian Utambule, alisema alitoia ekari mbili na kupatiwa fidia ya shilingi Milioni 3.6, ambazo aliweza kuongeza nguvu ya biashara yake ya duka.
Alisema pesa zilizobakia aliweza kufanyia kazi za kilimo kwa kulima zao la mpunga na kupanda ekari nne, huku akinufaika na kupatiwa fedha katika kikundi chao cha ushirika.
“Nashukuru pia fedha nyengine niliweza kulipia ada watoto wangu skuli, nyengine nikawanunuia vifaa vya skuli kwani wapo wanaosoma sekondari na wengine wanasoma msingi,”alisema.
Kwa upande wake Mrashi Jumbe Dongwa kutoka kijiji cha Sanjo kata ya Mkula, alisema baada ya tathmini kupigwa mara ya kwanza katika shamba lake yenye ukubwa wa ekari mbili (2) alilipwa Milioni 11.5 ambapo halikua na mazao, mara ya pili (2) alilipwa Milioni 12.6 ikiwa ni robo tatu shamba likiwa na miwa.
Alisema binafsi fedha hiyo aliweza kugawana na wanafamilia wenzake, ambao wanamiliki mashamba hayo na fedha zake kuzutumia katika kununua shamba jengine na kuwekeza kilimo jambo ambalo hakupata hasara kwao.
Mtendaji wa kijiji cha Sole Wendo Isdory alisema tayari wananchi wameshalipwa fidia ili kupisha mradi wa ushoroba, huku baadhi yao fedha hizo walinunulia mashamba na wengine kuekeza kukuza biashara zao za maduka.
naye Meneja wa Shoroba, kutoka Mpango wa kuhifadhi Tembo kusini mwa Tanzania (STEP) Joseph Mwalugelo, alisema baada ya wananchi kukubali kufanyiwa tathmini katika mashamba yao, tathmini iliangalia ardhi, mazao yaliyopo shambani au vibanda, jumla ya shilingi Bilioni 1.7 zililipwa kwa vijiji vitatu vilivyopitiwa na mradi wa shoroba mwaka 2022.
Aidha alivitaja vijiji ambavyo vimelipwa fedha hizo kuwa ni Mangula A, Sole na kanyenja, kwa mashamba 179, ambapo STEP walilipa kwa kutumia wafadhili mbali mbali.
“Baada kuidhinishwa tu kabla ya miezi sita tuliweza kulipa fedha zoet, laiti kama ingechelewa ingekua hasara kwetu,”alisema.
Hata hivyo alisema tayari wameshafanya tena tathmini kwa watu waliokuwa wanaumwa au hawakuwepo na wengine walikuwa mbali, ambapo Jumla ya shilingi Milioni 261 kwa watu 52.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa JET John Chikomo, aliwataka waandishi kuhakikisha waandika habari zitakazosaidia jamii, na sio jamii kumuona mnyama tembo kama ni aduwi kwake, bali ni kivutio kikubwa kwa taifa katika sekata ya utalii.