NA ABDI SULEIMAN.
Afisa Mdhamini Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Pemba Abdull-wahab Said Bakari, amesema miongoni mwa malengo ya serikali ya SMT na SMZ ni kupunguza umaskini kwa wananchi na kuongeza kasi ya ukuwaji wa uchumi.
Alisema serakali imepanga mpango wakupunguza umaskini na kuongeza ukuwaji wa uchumi jumuishi, ndio maana TASAF imewekeza kila sifa kwa walengwa wake.
Mdhamini aliyaeleza hayo wakati akifungua mafunzo kwa masheha na madiwani wa Mkoa wa Kusini Pemba, juu ya kuwajengea uwezo viongozi wanaosimamia shuhuli za Mpango wa kunusuru kaya masikini Tanzania, Mkutano ulioandaliwa na TASAF Pemba na kufanyika mjini Chake Chake.
Alisema matumaini ya TASAF kwenye mafunzo hayo, masheha watakua ndio masikio mazuri ya TASAF kwa kusikiliza changamoto za walengwa wa mpango na wanakabiliana nazo.
“Hivi sasa kume na changamoto nyingi nyinyi kutoka kwa walengwa, masheha na madiwani mutakuwa ni mabalozi, pia mutakuwa ni wasemaji wazuri wa kuisema TASAF kwa jamii,”alisema.
Aidha alisema Changamoto kubwa tutazifikisha kwa watendaji ili kupatiwa ufumbuzi, yale maneno ambao sio sahihi yataweza kupatiwa ufafanuzi, ili changamoto zinazotokezea za wananchi zinahitaji kutatuliwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Tanzania, Mkurugeni Uratibu TASAF Haika Shayo, alisema mfunzo hayo yatasaidia kufanikisha lengo la mpango, kwani kutakua ni mwanzo mzuri kwa viongozi hao kufahamu kikamilifu juu ya masuala na shuhuli mbali mbali za TASAF.
“Sote tunafahamu lengo ni kuwa na uwelewa wa pamoja na kuweza kuwahudumia walengwa, mutakuwa mabalozi wa mpango kwa kuwafahamisha wananchi wetu pale wanapokuja katika shehia zenu,”alisema.
Aidha aliwataka viongozi hao kuwa mabalozi wazuri wa mpango, huku wakiwahimiza walengwa kuhakikisha wanafungua akaunti benk kwa ajili ya kupokea fedha zao, kwani suala la fedha fedha mkononi limeshaondoka,”alisema.
Naye afisa Ufuatiliaji TASAF Pemba Abrahman Khamis, madhumuni ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo viongozi hao wanaosimamia shuhuli za mpango, kuwa na uwelewa wakutosha juu ya taratibu zinazotumika kusimamia na kufuatilia shuhuli za Mpango.
Alisema madhumuni mengine ni kufahamu majukumu sheha na kamati za usimamizi za jamii (CMC)katika shuhuli za mpango muda wote unapokua.
Mratib wa Tasaf Pemba Mussa Said alisema lengo ni kuongeza kipato kwa wananchi, pamoja na kuongeza ujuzi kupitia miradi wanayoianzisha kwenye shehia zao.
Alisema ushirikishwaji wananchi ni jambo kubwa katika kuibua miradi ya maendeleo ya sheria kupitia walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini.
Kwa upande wao masheha wameahidi kwenda kusimamia kikamilifu, shuhuli zote za TASAF zinazopofika katika shehia zao, kwani wao ndio viongozi wa serikali kwenye shehia husika.
MWISHO