Friday, November 15

ZEMA yateketeza tani 1.5 ya vifuko vya plastiki Pemba

NA ABDI SULEIMAN.

MAMLAKA ya Usimamizi wa Mazingira Pemba, imefanikiwa kuteketeza kwa moto Tani 1.5 ya vifuko vya plastiki vikiwa na Thamani ya Zaidi ya shilingi Milioni 10, mali ya mfanya biashara Mohamed Juma Ali wa Kiuyu Minungwini.

Zoezi la utekelezaji wa vifu hivyo lilifanyika huko huko kwareni Vitongoji nje kidogo ya mji wa Chake Chake, huku likisimamiwa na viongozi mbali mbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uchomaji huo Moto, katimu Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Pemba, Shaib Mohmmed Abdalla aliwataka wafanyabiashara kutii ambri ya serikali kwa kuachana na biashara ya vifuko ambavyo vimekatazwa kisheria kutumika ndani ya Visiwa vya Unguja na Pemba.

Alisema vifuko hivyo vimekua vikiharibu mazingira, hivyo wataendele kuhamaisha doria na kuhakikisha wanauteketeza mtandao mzima wa biashara hiyo.

Naye mkuu wa divisheni ya ufuatiliaji na Operesheni za Mazingira kutoka ZEMA Pemba Said Mbarouk Juma, alisema mifuko hiyo imekamatwa 16/3/2023 kiuyu Minungwini na kupelekwa mahakami Machi 20 na kuhukumiwa, kwa kutakiwa kuteketezwa kwa moto.

Alisema mifuko hiyo imepigwa marufuku nchini, kwa sheria ya Mazingira 2015 na kanuni zake za 2018 ya udhibiti ya mifunko ya plasti, kwa wale wanaotumia, wanaingiza, wanahifadhi, kuuza na  kusambaza.

“ZEMA imekua ikijitahi kufuatilia mifuko hiyo, ila wafanyabiashara wamekuwa ni wakaidi na kusahau kuwa mifuko hiyo ni hatari kwa maisha ya binaadamu,”alisema.

Aidha aliwataka wafanyabiashara kuachana na biashara hiyo ya mifuko ya plaski, ZEMA imekusudia kuteketeza mtandao mzima wa uingizaji wa vifuko hivyo kila watakapovikamata, bila ya kuangalia ukubwa wa mfanyabiashara,”alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya mazingira Pemba Mwalimu Khamis Mwalimu, alisema vifuko vya plastiki ni kemikali mbali mbali, ambazo bianaadamu zinaweza kumuathiri kwa kiasi kikubwa iwapo atatumia vifuko hivyo.

“Hapa kuna athari mbali mbali zinazopatikana katika mifuko hiyo, ikiwemo kiafya kwa wale watakoweka kitu moto kama vile maziwa, au vyakula na nyengine ni athari za kimazingirana,”alisema.

Aliwataka wafanya biashara kuachana na tamaa ya kuendelea kuathiri familia zao, ndugu zao kwa kuingiza mifuko hiyo badala yake kuingiza mifuko rafiki ya mazingira ikiwemo mifuko ya karatasi au mikoba ya ukili.

MWISHO