Monday, November 25

BENK ya NMB yafutarisha wateja wake Pemba

 

  NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.

UONGOZI wa Bank ya NMB tawi la Chake Chake Pemba, umejumuika pamoja na wateja wake Kisiwani humo katika futari ya pamoja huko katika hoteli ya Sunset wesha Kisiwani Pemba.

Akizungumza baada ya dhifa hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, alisema kuwa uongozi wa Serikali ya Mkoa huo unathamini sana mchango unaotolewa na NMB katika huduma mbali mbali na iko pamoja katika kushirikiana na Bank hiyo.
Mjaja alifahamisha kuwa kitendo kilichofanywa na Uongozi wa Benki hiyo ni Kikubwa sana ambapo  kwa kula futari hiyo sio jengine bali ni kuwakutanisha pamoja Ili kujuana  na kupata Fadhila kwa ujumla.
“Tunaupongeza sana Benki ya NMB Kwa dhifa hii adhimu waliyotukorimu na kuitaka kuendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wananchi kwa ujumla katika shughuli mbali mbali za kijamii,” alieleza Mjaja.
Sambamba na hayo,Mkuu huyo wa Wilaya alifahamisha kuwa NMB haishughuliki na utoaji wa huduma za kifedha kwa wateja wake, bali imekuwa ikishughulika na kazi nyengine za kijamii ikiwemo kuwakutanisha watu na makundi mbali mbali, ili waweze kukaa pamoja, kufanya shughuli zao na kutambua NMB ni kama Benki nyengine ambazo zinafanya kazi zake hapa nchini.
“Sisi wananchi wa Kisiwa Cha Pemba tunathamini sana mchango ambao unatolewa na ndugu zetu wa NMB na tuko pamoja katika kushirikiana nao,” alieleza Mjaja.
Mapema Mjaja alitanabahisha kuwa kitendo cha kuwafutarisha watu katika mwezi mtukufu wa ramadhani ni kitendo kizuri ambapo hata katika vitabu vitukufu viagiza jambo hilo.
Akitoa Salamu za Benki hiyo Kwa waumini hao, Meneja Mwandamizi wa NMB Ali Ngingiti alieleza kuwa katika mfungo wa Ramadhani NMB imekuwa ikijimuika na wateja wake na wadau wao mbali mbali katika kufutari pamoja kwani Wanaamini kuwa mwezi wa ramadhani Imani zao.
Aidha Ngingiti aliwasisitiza waumini hao kuendelea kukumbushana juu ya kutumia mwezi mtukufu wa ramadhani kutafakari upendo wa dhati Kwa Mwenyezimungu na kuimarisha Imani zao.
“Niendelee kuwasihi waislamu wote  nchini na ulimwenguni Kwa ujumla kutumia mwezi huu Kwa kujiweka karibu na Mwenyezimungu na kuimarisha Imani zetu sawa sawa,” alifahamisha Ali.
Sambamba na hayo Ali aliwataka wadau hao kuendelea kutenda mema,kuvuta uradi na kuweza kuendelea kuswali katika kipindi kilichobaki na hata baada ya mwezi mtukufu wa ramadhani kumalizika.
Nae Meneja wa NMB tawi la Chake Chake Pemba Hamad Msafiri aliwataka wateja wa NMB kuendelea kutoa mashirikiano yao Kwa Benki hiyo na kusema kusema kuwa NMB ni salama Kwa ajili ya kufanya shughuli zao za kifedha.
“Niwashukuru sana wateja wetu Kwa kukubali kuwa nasi katika hafla yetu hii, ninawaambia ahsanteni sana ,” alieleza Msafiri.
             MWISHO.