Thursday, January 30

Wadau wakutana kupitia rasimu ya uchambuzi wa hali halisi ya sera ya msaada wa kisheria ya mwaka 2017.

 

NA ABDI SULEIMAN.

AFISA Mdhamini Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora Pemba Halima Khamis Ali, amesema lengo la kukusanya maoni ya Rasimu ya Uchambuzi wa hali halisi ya sera ya msaada wa Kisheriaya Mwaka 2017, ni kwenda sambamba na mabadiliko ya dunia katika utoaji wa msada wa kisheria kwa wananchi.

Alisema hivi sasa mambo mengi yamebadilika hivyo na watoa msaada wakisheria wanapaswa kubadilika katika utoaji wa elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi, kwa kuhakikisha hata vijijini wananchi wanapatiwa elimu hiyo.

Hayo aliyaeleza wakati akifungua mkutano wa wahusika (wadau) wa kukusanya maoni ya Rasimu ya Uchambuzi wa hali halisi ya sera ya msaada wa Kisheriaya Mwaka 2017, mkutano uliofanyika mjini chake chake.

Alisema sera hiyo itakapopitishwa itaendana na mazingira rafiki yaliyopo, wadau wanawajibu wakuitendea haki na kuhakikisha sera hiyo inaondosha changamoto zilizojitokeza katika sera iliyopita.

Sisi wadau kazi yetu ni kuona sera hiyo inapitishwa kwa nguvu zote, hivi sasa dunia imebadilika katika mambo mbali mbali vizuti kupitishwa na kufanya kazi,”alisema.

Mapema Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar Hanifa Ramadhan Said, alisema changamoto kubwa wananchi kutokua na watu wa kusimama nao mahakamani baada ya kuhamasika vijijini, kupatiwa elimu na watoa msaada wa kisheria.

“Wasaidizi wa sheria ndio wanaofika vijijini na kuibua changamoto za wananchi na kuhamasika kufungua kesi mahakamani, lakini wanashindwa kupata haki zao kwa kutokua na miguu ya kusimama mahakamani,”alisema.

Alisema idara imeona mambo mengi yametekelezeka, kila eneo lililohitajika katika sera kupitia wasaidia wa sheria, wameweza kutekeleza zaidi ya 80% wamejitokeza, lakini ipo haja ya kuanzishwa kwa mfuko wa msaada wakisheria ambao utaweza kuwasaidia mawakili.

Akitoa maelezo mafupi ya Rasimu ya Uchambuzi wa hali halisi ya sera ya Msaada ya kisheria ya mwaka 2017, kwanasheria kutoka taasisi ya Msaada wa kisheria na Haki za Binaadamu Halfan Amor Mohamed,alisema ipo haja ya kua na sera mpya ya msada wakisheria, kwani sera ilyopo sasa imekamilisha kila kitu.

Aidha mshauri huyo alipendekeza kuwepo na mfuko maalumu wa msaada wakisheria utakaoweza kusaidia mawakili kusimama mahakamani na kusikiliza, pamoja na idara ya katiba na msaada wakisheria Zanzibar kuanzisha kitendo cha tathamini na ufuatiliaji.

Akichangia maoni Salum Makame Ali, alisema wasaidizi wa sheria wamejitahidi sana kutoa elimu kwa wananchi ambao walikua wakihitaji msaada wa kisheria.

Naye Rashid Hamad Ali kutoka Chuo cha Mafunzo Pemba, alisema haoni umuhimu wakupatikana kwa sera mpya, kwani sera iliyopita inahitaji kufanyiwa marekebisho madogo madogo yaliyopo.

MWISHO