NA ABDI SULEIMAN.
JUMLA ya Miti 1,573,669 ya aina mbali mbali ikiwemo matunda, mikoko na Viungo Imepandwa katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Machi 2023.
Ambapo Wilaya ya Wete miti 1,387,313 kati ya hiyo miti 1,319,000 miti ya mikoko (mikandaa) na 68313 miti ya matunda, Viungo na misitu.
Kwa Wilaya ya Micheweni jumla ya miti 189,356 imepandwa, kati ya hiyo miti 108,431 miti ya mikoko (mikandaa), na miti 80,925 miti ya matunda, viungo na misitu.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, alisema lengo la upoandaji wa miti hiyo ni kuitikia ujumbe wa mwenge “Tunza mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai kwa Uchumi wa Taifa” na kufikia kupanda miti hiyo.
Mapema Mkimbizaji wa mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Abdalla Shaibu Kaimu, aliwataka wananchi kuendelea kupanda miti kwa wingi, ili kuhifadhi mazingira.
Alisema mabadiliko ya tabianchi yamekua yakiendelea kutokea siku hadi siku hivo, suala la upandaji wa miti linapaswa kua endelevu ili kurudisha uwoto waasili uliopotea.
Afisa Mdhamini Wizara ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Pemba Mhandisi Idris Hassan Abdalla, alisema eneo la kishindeni shehia ya Mapofu Wilaya ya Micheweni kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023 jumla ya miti 190,856 sawa na hekta 2,463.19 ilioteshwa katika maeneo mbali mbali.
Alisema miti 67,750 ya misitu eneo la hekta 27.1, miti 104,431 ya mikandaa sawa na eneo la hekta 2,377, miche 5,055 ya mikarafuu sawa na hekta 50.55, miche 1,200 ya minazi sawa na hekta 7.7 na miti ya mikaratusi 8,420 sawa na eneo la hekta 0.84.
Aidha alisema katika eneo la kishindeni kazi ya uhifadhi wa mazingira ulianza kutekelezwa mwaka 2020 baada ya kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa mazingira katika eneo hilo kutokana na uchotaji wa mchanga uliokua unafanyika kwa matumizi mbali mbali.
“Lengo kuu la mradi huu ni uhifadhi wa mazingira pamoja na kuotesha michez ya biashara katika naeno hili ambalo lilikuwa limeanza kubadilika na kuwa jangwa,”alisema.
Alifahamisha kwa kushirikisha na shirika la biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) miti ya mikaratusi 1,500 ilipandwa na kufikisha idadi ya miti 8,420 ya aina hiyo kupandwa eneo lenye hekta 0.84 msimu wa masika.
Aliongeza kuwa upandaji wamiche hiyo inafaisa kubwa katika uhifadhi wa eneo hilo, ambapo miti hiyo itatuka kwa jili ya kuvuna majani yake ambayo hutumika katika uzalishaji wa mafuta na kusaidia kuongeza pato la taifa.
Hata hivyo alisema tayari jumla ya miche 88,420 imeshaoteshwa katika neo la kishindeni sawa na ukubwa wa hekta 8.42 yenye thamani ya shilingi 1,768,400,000.
Kwa upande wa mashindeni shehia ya Kangagani Wilaya ya Wete, jumal ya miti 7,500 imeshapandwa kwenye shamba lenye ukubwa wa ekari 2.83, ikiwemo mikeshia 6,750, mivinje 700 namiarubaini (mitunda)50.
MWISHO