Thursday, November 14

Vijana watakiwa kutambua thamani yao na kuachana na migogoro ya kisiasa.

NA ABDI SULEIMAN.

AFISA Mdhamini Wziara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau, amesema vijana sasa hivi wamekuwa wanapitia mambo mengi, hivyo elimu ya amani wanapaswa kupatiwa mara kwa mara ili kuendelea kuwa vijana wema kwa taifa lao.

Alisema vijana waliowengi wanamekuwa wakijihusisha na migogoro ya kisiasa, kutokana na kushawishiwa na wanasiasa hivyo wanapaswa kutambua thamani yao katika nchi ni ulinzi na utunzaji wa amani.

Mfamau aliyaeleza hayo huko katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Micheweni, wakati akizungumza na vijana baada ya kumalizika kwa mafunzo yaliyotolea na CYD, kupitia ufadhili wa UNDP.

Aidha aliwataka viojana kuhakikisha wanafanya kazi ili kujisaidia wao na familia zao na sio kukaa barazani, kwani taasisi nyingi zinaendelea kuwapatia elimu mbali mbali.

“Kumekua na mashirika mengi yanayojuka kuwasaidia vijana kwa kuwapatia taaluma, ikiwemo ufundi na elimu nyengine ili muweze kufikia malengo yenu, niwakati sasa kuhakikisha elimu hiyo kwa vijana wenzenu,”alisema.

Aidha alisema ni wakati sasa kwa vijana kutumia fursa ya kuhamasisha suala la amani, kufanya hivyo watakuwa wameishaisaidia serikali kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake Mkufunzi kutoka Jeshi la Polisi Inspekta Hasshin Ali Hashim, alisema vijana waliongi wanashindawa kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya shuhuli zao za maendeleo.

“Mitandao ya kijamii utakavyoweza kuitumia vizuri basi tutaweza kufanikiwa kutokana na fursa ningi zinazokuja kwa kuwasiaidia vijana, kufikia ndoto zenu za kimaisha,”alisema.

Hata hivyo aliwataka vijana kutokukubali kuyumbishwa na wanasiasa, badala yake wanapaswa kuwa mstari wambele katika kulinda na kudumisha amani iliyopo nchini.

Mkurugenzi wa CYD, Hashima Pondeza, alisema mradi umekuja kwa ajili ya kuwasaidia vijana, kwani imeona vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika makundi maovu ambayo yanahatarisha usalama wao.

Alisema vijana wengi katika Wilaya ya Michweni wamekuwa wakikimbilia nchi jirani, baada ya kufanya mambo ambayo hayafai wala hayaendani na mila silka na tamaduni.

“Vijana wananafasi kubwa ya kuhakikisha amani na utulivu inadumu muda wote ndani ya mioyo ya vijana wenzao na wananchi kwa ujumla,”alisema.

Afisa Vijana Wilaya ya Micheweni Yunus Bakar, alisema vijana wamekua na mwamko mzuri katika suala zima la mendeleo hivyo wanapaswa kuendeleza umoja na mshikamano wao.

MWISHO