Thursday, November 14

CYD yawakutanisha vijana kutoka Wilaya ya Wete na Micheweni katika kupanga mpango kazi wa kuwasaidia na kuchagua miradi 

NA ABDI SULEIMAN.

VIONGOZI wa Wilaya ya Wete na Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba wamesema katika siku za hivi karibuni Vijana wengi wameweza kubadilika tabia kwa kiasi kikubwa hali inayowafanya kuondokana na mfumo wa kuchaguliwa miradi ya maendeleo.

Wamesema vijana Sasa wamekua wabunifu wakubwa wao wenyewe katika kuchagua miradi inayoendena na wao na kuwa rahisi kwao kutekeleza na kupata mafanikio makubwa.

Wakizungumza katika mkutano wa kupanga mpango kazi wa kuwasaidia na kuchagua miradi itakayotekelezwa na vijana 15 kutoka Wilaya ya Wete na Micheweni 15, kupitia mradi wa Dumisha Amani unaotekelezwa na kituo Cha majadiliano Kwa Vijana Zanzibar (CYD) na kufanyika mjini chake Chake.

Katibu Tawala Wilaya ya Micheweni Sheha Mpemba Faki, alisema vijana wamebadilika na kuchagua miradi yao wenyewe ambayo wanaweza kutekeleza ipasavyo bila ya vizingiti vyovyot.

“Vijana ndio wanaotekeleza miradi hiyo katika maeneo yao na baadae ya kuchagua au kupatiwa na wahisani, Sasa haipendezi kuchaguliwa vizuri kuchagua wenyewe miradi hiyoo ili iwe rahisi kiisimamia”alisemaa.

Aidha alisema serikali za Wilaya zinapaswa kuwasaidia vijana hao kupata usajili wa haraka haraka ili waweze kufanikiwa na katika mradi huo wa Dumisha Amani kwa Vijana.

Nae Katibu Tawala Wilaya ya Wete Mkufu Faki Ali,  alisema taasisi ya CYD imeweza kuwasaidia Kwa kiasi kikubwa wananchi wa Wilaya ya Wete hususan kupitia mradi wa Dumisha Amani na mradi wa Amani Mipakani, ambao umewasaidia sana vijana katika miradi hiyoo.

Alisema vijana wapo ambao wamenufaika na shuhuli za kilimo, mifugo, ushoni hivyo kupitia mradi huo watahakikisha wanafanikiwa Kwa kiasi kikubwa katika miradi yao watakayoibua.

“Sisi hapa Wete wapo vijana wengi wamefanikiwa kupitia miradi iliyoletwa na CYD na Sasa wamefanikiwa, Sasa hivi kila siku tunapata taarifa kutoka Kwa Vijana wetu juu ya kinachoingia baharini,”alisema.

Hata hivyo aliwataka vijana wa Wete, kujikita katika suala la utoaji wa elimi katika shehia ya Kizimbani kwani kumekua na matukio mengi ya vijana ambao wanakoelekea sio kuzuri katika suala Zima la kudumisha Amani Nchini.

Mapema mratibu wa CYD Pemba Ali Shaban Mtwana, alisema katika utekelezaji wa mradi imefikia hatua Sasa  katika kuwasaidia vijana 30 katika kubuni miradi miradi ambayo itaweza kuwasaidia wao na kuendeleza kutia elimu ya Dumisha  Amani mitaani na Kwa vijana wenzao.

“Kila Wilaya itakua na kikundi Cha watu 15 wale ambao tumekua tukiwa nao katika mradi wetu, vijana hawa wataweza kubuni miradi yao ya pamoja na sio ya mtu mmoja mmoja, hapa mukiwa wengi ndio mutaweza kufanya vizuri,”alisema.

Kwa upande wake mratibu wa idara ya Maendeleo ya Vijana Pemba Ali Mussa Bakar, alisema utekelezaji wa mradi huo Kwa vijana ni utekelezaji wa Ajira laki tatu zilizoahidiwa na Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi, pamoja na idara katika kuwasaidia vijana nchini.

Alisema CYD inamiradi mingi inayosaidia vijana hivyo lazima tuithamini kwani imekua ikisaidia kwa kiasi kikubwa  serikali katika kuwapatia elimu na miradi mbali mbali ya maendeleo.

Hata hivyo nao vijana wamewataka Viongozi wa Wilaya na Wizara ya Habari Vijana utamaduni na Michezo, kuhakikisha wanawasaidia vijana katika suala zima usajili wa kikundi na ufunguaji wa akaunti benk, ili kuwapunguzia gharama.

MWISHO